TATIZO LA CHUPA YA UZAZI KUPASUKA MAPEMA KABLA YA WAKATI(PREMATURE RUPTURE OF MEMBRANE(PROM))

 CHUPA YA UZAZI KUPASUKA MAPEMA


Hii ni mojawapo ya dalili za hatari kwa mama mjamzito ambapo kwa kitaalam huitwa premature rupture of membrane(PROM), Hivo basi endapo mjamzito kakutana na hali hii ni bora sana kukimbilia hospital kwa ajili ya kupata msaada zaidi.


BAADHI YA SABABU ZA CHUPA YA UZAZI KUPASUKA MAPEMA


- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali au Infection kama vile za,UTI, FANGASI,PID, Kaswende(syphilis), N.K


- Kupatwa na shida ya kuanguka au kupigwa wakati wa ujauzito


- Hali ya maji kuwa mengi sana katika tumbo la uzazi hivo kupelekea mgandamizo au presha kubwa ndani ya tumbo la uzazi(polyhdrominous)


- Uwepo wa watoto zaidi ya mmoja tumboni(multiple pregnancy), kama vile mapacha, watoto watatu N.K


KUMBUKA; mama ambaye chupa ya uzazi imeshapasuka yupo katika hatari ya kupata maambukizi mengine ambayo huweza kupenya na kupita moja kwa moja kwenda kwa mtoto aliyetumboni na kumsababishia madhara makubwa.


Inashauriwa mama baada ya kupatwa na shida hii ya chupa kupasuka mapema,azalishwe  mapema ili kumuokoa yeye na mtoto aliyetumboni pia.



Kwa Ushauri zaidi,elimu au tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584 tuma ujumbe au piga simu utasikilizwa na kusaidiwa.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!