TATIZO LA GIANT CONGENITAL MELANOCYTIC NEVUS



Baadhi ya watoto huzaliwa na tatizo linaloitwa Giant Congenital Melanocytic Nevus (GCMN),ambalo hutokea siku za mwanzo kabisa za utungwaji wa ujauzito kutokana na changamoto za mabadiliko yasiyo ya kawaida ambayo chembechembe za urithi huzipitia (NRAS & BRAF gene mutations). Hutokea kwa wastani wa mtoto mmoja katika kila watoto 20,000 wanaozaliwa duniani. Changamoto hii inayoambatana na kutokea kwa makovu makubwa yenye rangi nyeusi huonekana tangu kuzaliwa kwa mtoto na huendelea kukua kadri umri wa mtoto unavyozidi kuongezeka. 

-

Tatizo hili huambatana na changamoto nyingi za kisaikolojia kwa mhusika,wasiwasi,stress na wakati mwingine hutengeneza mgandamizo mkubwa kwenye ubongo hivyo kusababisha maumivu makali ya kichwa,kutapika,kulialia kila mara,kifafa pamoja na uvimbe mkubwa kwenye ubongo

-

Tatizo hili linatibika kabisa. Watoto wenye changamoto hii wasaidiwe,wapelekwe hospitalini ili watibiwe. Njia kuu ya matibabu yake ni upasuaji.

Pangusa picha kuona tofauti ya mtoto huyu kabla na baada ya kutibiwa.

Via afyainfo 

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!







0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!