Tatizo la kuharisha huondoa uhai wa watoto wengi sana duniani. Husababisha upotevu wa maji na chumvichumvi muhimu za mwili. Watoto wanaoharisha hulegea sana,huishiwa nguvu,hulialia kila muda,huhangaika bila sababu na macho yao huingia ndani.Katika mazingira ya kawaida tatizo hili linaweza kudumu kwa siku moja au mbili hivi
-
Ukiona mwanao anaharisha mfululizo kwa zaidi ya siku 2 inapaswa umuwahishe hospitalini haraka sana. Athari za tatizo hili ni kutokea kwa homa kali,kupotea kwa hamu ya kula,kupoteza uzito na kutokana na upoteaji wa maji mengi na chumvichumvi unaotokea,mtoto huyu anaweza kupata kifafa,matatizo kwenye ubongo pamoja na kifo. cc.afya-info
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!