UWEPO WA TATIZO LA KUTOKA USAHA KWENYE UUME WAKATI WA KUKOJOA
Tatizo la Kuwepo kwa chembechembe za usaha au usaha kwenye mkojo hujulikana kama pyuriaambapo linaweza kuonekana kwa kutumia hadubini (microscope) au kama tatizo ni kubwa linaweza kuonekana kwa macho.
•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake
🔻VISABABISHI VYA TATIZO HILI LA KUTOKWA NA USAHA KWENYE UUME
Zipo sababu mbalimbali ambazo huchangia sana kutokea kwa hali ya kutokwa na usaha kwenye uume wakati wa kukojoa,ambapo ni pamoja na;
- Ugonjwa au maambukizi katika mfumo wa mkojo yaani UTI ambapo huhusisha Maambukizi kwenye figo, kwenye mrija wa mkojo na kwenye kibofu cha mkojo (cystitis- amabayo huonekana sana)
- Magonjwa ya Zinaa-Kama ugonjwa wa kisonono au ‘’gono’’ kama wengi wanavyoita, ugonjwa wa Chlamydia na Trichomoniasis
- Sumu inayotokana na kemikali (Chemical poisoning) kama 4-Aminodiphenyl inayotumika kwenye maabara kwa ajili ya tafiti mbalimbali
- Tatizo linajulikana kama Reiter’s syndrome
- Pyelonephritis-Maambukizi ya bakteria kwenye sehemu za figo zinazojulikana kama calyces, renal pelvis na tishu za figo .Madhara ya pyelonephritis ambayo husabababisha ugonjwa unaojulikana kama renal abscessMl
- Maambukizi kwenye tezi dume-Prostatitis (Kwa wanaume)
- Upungufu wa kinga mwilini
- Uvimbe kutokana na kuwepo kwa mawe kwenye kibofu cha mkojo au kwenye figo
- Mzio (Allergy) au kuota uvimbe sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo
📶 DALILI ZA UWEPO WA TATIZO HILI
Viashiria vya tatizo hili pamoja na dalili zake ni Pamoja na;
-Maumivu makali ya kuchoma (Painful burning sensation) wakati wa kukojoa
-Maumivu chini ya kitovu
-Homa
-Kutapika
- Usaha kutoka wakati wa kukojoa
-Tatizo hii likidumu kwa muda mrefu husababisha kupungua uzito kwa mgonjwa
Cc:afyadarasa #afyaclass
•Soma: Ugonjwa wa Tezi Dume, chanzo,Dalili zake pamoja na Matibabu yake
🔷 MATIBABU
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!