Ticker

6/recent/ticker-posts

TATIZO LA MAPUNYE KWA WATOTO



MAPUNYE

• • • • • •

MAPUNYE NI NINI?


Mapunye ni aina ya maradhi ya fangasi yanayoshambulia ngozi haswa ngozi ya kichwa. Mapunye kwa lugha ya kitaalamu huitwa “Tinea capitis”. Ugonjwa huu hushambulia watu wote wa jinsia na umri wote,ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo. Ugonjwa huweza kushambulia eneo lote la kichwa au sehemu tu ya kichwa, sehemu iliyoshambuliwa na mapunye huwa na umbo lililofanana na sarafu.


NAMNA YA KUAMBUKIZWA MAPUNYE 


1. Kutumika kwa vifaa vya kunyolea kw azaidi ya mtoto mmoja bila kuvifanyia usafi.


2. Kutumia taulo au nguo ya kujikaushia kwa mtoto zaidi ya mmoja, hasa pale ambapo mmoja wa watoto hao akiwa na maambukizi ya ugonjwa wa mapunye.


3. Kutumia vifaa vya nywele kama chanuo la kuchania nywele kwa zaidi ya mtoto mmoja.


4. Kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari.


•Soma: Ugonjwa wa Lawalawa kwa Watoto wadogo,chanzo,dalili na Tiba yake


JINSI YA KUMKINGA MTOTO DHIDI YA MAPUNYE


a) Usafi wa mwili wa mtoto kama kuhakikisha mwili haswa kichwa cha mtoto kinabaki na ukavu muda wote.


b) Hakikisha nguo, taulo na mashuka yanafuliwa kwa sabuni na maji yaliyo safi.


c) Kwa watoto wanaosoma shule za bweni ni vyema kuhakikisha watoto hawa wanaepuka kushirikiana katika utumiaji wa vifaa vya kufanyia usafi wa mwili mfano taulo.


d) Epusha kushirikiana vifaa vya kunyolea nywele na vifaa vya kuchania nywele haswa kwa watoto wanaosoma shule za bweni.


MATIBABU


Mapunye hutibiwa kwa dawa za kutibu magonjwa ya fangasi. Dawa hizi ni za kupaka, hii ni kwa kuwa ni rahisi kwa dawa ya kupaka kupenya kwenye ngozi na kusababisha matokeo yanayohitajika. 


Ni vyema zaidi dawa za mapunye kwa watoto kushauriwa na daktari kulingana na jinsi alivyoathirika na ugonjwa huo.


•Soma: Ugonjwa wa Lawalawa kwa Watoto wadogo,chanzo,dalili na Tiba yake


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments