MATITI
• • • • • •
Tatizo hili kitaalamu huitwa MASTITIS, Ni mcharuko mwili (inflammation) katika matiti ambao hutokana na maambukizi ya bakteria. Maambukizi haya hupelekea maumivu katika matiti. Huwatokea zaidi kina mama wanaonyonyesha (Lactation Mastitis)
DALILI NA VIASHIRIA
1. Maumivu katika matiti na hali ya umoto katika ngozi ya titi
2. Kuvimba matiti (si uvimbe wa kansa)
3. Maumivu makali yenye kuchoma wakati wa kunyonyesha
4. Wekundu wa ngozi ya titi
5. Homa kali
6. Kujihisi uchovu na kuumwa kiujumla
VISABABISHI (Causes)
1. Maziwa kutoka yote wakati wa kunyonyesha hivyo kupelekea njia za maziwa kugota (blocking). Mrundikano huu wa maziwa hupelekea maambukizi ya bakteria katika ziwa
2. Bakteria kuingia katika titi aidha kwa kupitia ngozi ama mdomo wa mtoto mama anyonyeshapo
VIHATARISHI (Risk factors)
1. Historia ya tatizo hili siku zilizopita
2. Chuchu zilizovimba ama kuchanika
3. Kuvaa sidiria/bra zinazobana kupita kiasi au kufunga mkanda wa gari kwa muda mrefu mno
4. Uchafu wa matiti (kutozingatia usafi wa matiti na usafi wa bra)
5. Lishe Duni
6. Uvutaji sigara .
.
HATARI/MADHARA
Mastitis huweza kupelekea JIPU (abscess) kwenye titi
NAMNA YA KUJIKINGA
1. Nyonyesha mpaka uone maziwa yameacha kushuka, usikatize hovyo
2. Muache mtoto anyonye titi moja mpaka Lishe kisha ndo umuhamishie titi lingine
3. Epuka uvutaji sigara
4. Zingatia usafi maeneo ya matiti
5. Usivae bra zinazobana mno haswa akina mama wanao nyonyesha
Cc.Drtareeq
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!