TATIZO LA MTOTO KUKOSA CHOO KABSA AU KUPATA CHOO KIGUMU

KUKOSA CHOO/KUPATA CHOO KIGUMU


- Kwa kawaida watoto wadogo hasa wale ambao bado wananyonya na ndyo kwanza wameanza kula vyakula vingine zaidi ya maziwa ya mama,hupata tatizo hili la choo kigumu au kukosa choo kabsa hali ambayo kitaalam hujulikana kama Constipation

- Hali hii huanza pale ambapo mtoto anapoachishwa maziwa ya mama na kuanza kupewa maziwa ya kopo au Ng'ombe,mara nyingi watoto wanaoendelea kunyonya maziwa ya mama hawasumbuliwi na hali hii.

- Hata hivyo,inaelezwa kwamba, kwa mama ambaye anasumbuliwa na tatizo hili la kukosa choo au kupata choo kigumu,basi huenda pia na mtoto akasumbuliwa na tatizo hili.

- Mtoto mwenye tatizo la kukosa  choo mara nyingi huanza kupata choo kigumu,tena kwa shida,huku akisumbuliwa na maumivu ya tumbo.

- Hali hii pia huchangia wakati mwingine mtoto akipata choo,hujiminya tumbo na kukunja uso.

- Unachotakiwa kukifanya pindi unapoona hali hii kwa mtoto wako ni kumuona daktari,hasa hasa kwa mtoto ambaye ana umri wa chini ya mwezi mmoja na hapati choo kwa Siku 4 na kuendelea. Cc.afyasolution

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!