TATIZO LA NGOZI
• • • • • •
Ngozi ya binadamu huwa na utaratibu wa kujiumba upya walau kila baada ya siku 27. Huu ni muda ambao ngozi mfu huondolewa na ngozi mpya ambayo huendelea kuunawirisha mwili wa binadamu. Haya ni mabadiliko yasiyoonekana kwa macho ya kawaida,lakini huwa yapo
-
Baadhi ya binadamu huzaliwa na tatizo la kurithi ambalo huitwa Ichthyosis vulgaris. Tatizo hili huifanya ngozi ishindwe kuziondoa seli za ngozi zilizokufa ili seli mpya za ngozi zipate nafasi ya kuendeleza kuimarisha afya ya ngozi. Ngozi ngumu,iliyo na magamba ambayo wakati mwingi huchanika huwasumbua sana watu hawa,kwa maneno ya mitaani ugonjwa huu huitwa “ugonjwa wa magamba ya samaki” kwa kuwa huwa na muonekano unaoshabihiana na kitoweo hiki
-
Tatizo hili linaweza kuonekana mwili mzima,au kwenye viungo fulani na huongezeka ukubwa wake hasa kwenye kipindi cha kiangazi wakati wa hewa kavu na jua kali. Ukubwa wa tatizo hili hutofautiana kati ya mgonjwa mmoja na mwingine lakini wengi wa wagonjwa hawa husumbuliwa na maumivu makali sana hasa kutoka kwenye sehemu za ngozi iliyochanika
-
Kwa bahati mbaya sana ugonjwa huu hauna tiba ya kudumu hadi sasa. Msaada wa kupunguza maumivu na ukubwa wa tatizo hutolewa kwa mgonjwa ili kufanya afurahie maisha yake kwa kipindi chote awapo duniani. cr.afyainfo
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!