TIBA YA HARUFU MBAYA KINYWANI UKIWA NYUMBANI KWAKO

HARUFU MBAYA MDOMONI

• • • • • • 

Zifuatazo ni baadhi ya tiba ambazo ni rahisi kuandaa mwenyewe ukiwa nyumbani na hazina madhara kabisa kiafya.


1. MBEGU & Kahawa (COFFEE BEANS)

Kutafuna karafuu, au hiliki, shamariand (fennel), mbegu za anise, mara moja huondoa harufu mbaya mdomoni.Kama unahisi unatatizo la aina ya vyakula kwa sababu ya meno, kuwa makini na hizi pia.Kula kahawa(coffee beans) ilo kaushwa ni nzuri zaidi na huondoa harufu mbaya.


2. NDIMU

Kulamba ndimu au kutafuna ganda dogo la ndimu ni nzuri kwa kuondoa harufu mdomoni pia.Lakini juisi ya ndimu ina acid na huweza kuwa mbaya kwa meno yako, husababisha meno kupata ganzi.


3. JUISI YA SIKI YA APPLE

Ni nzuri! Sio tu kwa ajili ya kusukutua ½ kijiko cha chai cha juisi ya siki ya apple iliochanganywa na kikombe cha maji,husaidia harufu pia,huondoa harufu ya vitunguu na huwa ni ladha pia ulimini.Kuchanganya na maji,huondoa ule ukali wake na utausikia mdomo uko vizuri mwepesi.Naifanyia kazi post zijazo kuhusu juisi ya siki ya apple na matumizi yake.


4. BAKING SODA

Kutengeneza mouthwashya baking soda na maji ni tiba ya asili ya muda mrefu. Tumia hii kwa kusukutua mara moja kwa siku.


5. MAJI

Pindi unywapo maji baada ya kula vitunguu au vitunguu thoum unaweza kuhisi haiondoi harufu na uchafu hapo hapo, kunywa maji mengi kwa mpangilio au utaratibu maalum husaidia mdomo kuwa fresh na harufu nzuri muda wote. Maji yanasaidia kuondoa bacteria wa kwenye chakula na huzidisha utengenezwaji wa mate kwa wingi, na pia huwa kama ni kiosha au kisafisha mdomo cha kudumu.

Harufu mbaya ya mdomo inakera ukiangalia vyakula vyenyewe hivi vya viungo na uzembe wa usafi unaoweza sababisha hata ukavu wa mdomo,vijidudu vya kwenye fizi, na vijidudu.Kama utagundua tatizo hili la harufu mdodmoni inaendelea,muone daktari wa meno kwa tiba na ushauri zaidi.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!