UGONJWA WA BUEGA (THROMBOANGIITIS OBLITERANS, BUERGER’S DISEASE)

🔻UGONJWA WA BUEGA (THROMBOANGIITIS OBLITERANS, BUERGER’S DISEASE)

➡️ Buega

Ni ugonjwa unaoshambulia mishipa ya damu ya ateri  ambayo huvimba,hupungua ukubwa wake na hata kuziba kabisa na kupelekea sehemu husika kukosa damu. Ugonjwa huu hushambulia mishipa midogo nay a saizi ya kati  ya damu ya miguu na mikono na kupelekea kuvimba,kupungua ukubwa wake na kupelekea mzunguko wa damu kwenda sehemu husika kupungua au kukata. 

Ugonjwa huu  kwa asilimia 99 husababishwa na matumizi ya bidhaa za tumbaku(tobacco products) kama sigara nk,ugoro nk,hio asilimia ilobakia inaweza kusababishwa na bangi(Cannabis arteritis).


🔷 WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU

1.Wanaovuta sigara kwa muda mrefu

2.Wanaume wenye umri chini ya miaka 50

3. Wanaovuta bangi

4. Wenye magonjwa ya muda mrefu ya fizi na meno(Chronic anaerobic periodontal infection).


📶 DALILI ZA UGONJWA WA BUEGA

➖ Kuvimba mishipa(Superficial thrombophlebitis ): hii ni mojawapo ya hatua ya mwanzo kabisa ya ugonjwa huu ambapo mishipa ya miguuni au mikono huanza kuvimba na kuuma,unaweza kuona kama mishipa inaanza kuonekana tofauti na mwanzoni na ukiishika inakua na vitu kama vinundu vinundu na inauma.

➖ Vidole kuhisi baridi sana(Raynaud phenomenon);Hii pia ni katika hatua za mwanzoni pia ambapo mgonjwa huhisi baridi sana kwenye vidole ,vidole hukaza,huonyesha ile michirizi ya baridi na kua vyeupe kwa maana mzunguko wa damu unakua mdogo,hali hii hutokea katika mazingirayeyote ya ubaridi au kushika vitu vya baridi.

➖ Vidole kua vya buluu(Digital ischemia):Kama mtu mwenye dalili za awali nlizotaja hapo juu akiendelea kuvuta sigara basi ugonjwa huzidi kuongezeka na kupelekea kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye vidole. Kupungua kwa mzunguko wa damu hupelekea vidole kubadilika rangi na kua vya buluu(Buerger's color);vidole kua vya buluu hupelekea vidole kuuma sana na kama hali ikizidi kuendelea basi vidole hufa(gangrene) na baade kutengeneza vidonda baada ya kufa(ukishafikia hali hii uwezekano wa kupoteza vidole au mkono au mguu ni mkubwa kwani ni lazima ukatwe ili kuokoa maisha yako)

➖ Matatizo ya viungo kama kuvimba,kuuma nk (Joint complaints)


🔻MATIBABU NA NAMNA YA KUJIKINGA NA BUEGA

Mpaka ninavoandika makala hii njia pekee ya kukulinda ama kupunguza muendelezo wa ugonjwa huu ni KUACHA MATUMIZI YA TUMBAKU  NA BANGI  KABISA(Complete abstinence of tobacco and cannabis use). Kufanya huivi kutakufanya ugonjwa uishe au kupungua na kukuondolea uwezekano wa KUKATWA MGUU AU MGONO. Hakuna tiba nyingine zaidi yah ii ya kuondoa tatizo hili.

Aidha mgonjwa wa buega atatibiwa kutokana na hali alokuja nayo mfano kama amekuja na vidonda basi vitasafishwa na kupewa dawa za kukausha,kama amekuja na matatizo ya viungo basi atapata matibabu ya viungo, kama kama na seheme ya mkono,kidole au mguu umesharibika sana au kufa basi tiba ni KUKATA MGUU AU MKONO(amputation).

MWISHO.

Cr: Dokta Mathew from Dodoma

 #afyaclass


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!