UGONJWA WA CORONA COVID19 NI NINI?
Huu ni ugonjwa wa kuambukiza ambao umesababishwa na kirusi aina mpya cha corona. Aina hii ya kirusi na ugonjwa ulianzia jiji la Wuhan, China mwezi Disemba 2019.
JE UGONJWA WA CORONA COVID19 UNASAMBAA VIPI?
Ugonjwa wa corona husambaa kutoka kwa mtu hadi mtu kupitia vitone vidogo vidogo vya mate vinavyoruka toka puani au mdomoni bali mtu mwenye maambukizi ya virusi vya Corona COVID19 anapopiga chafya , kukohoa au kupumua.
Vitone hivi vya mate huweza kutua kwenye nyuso za vitu hivyo watu wengine hupata virusi hivi wanapogusa hivi vitu. Vitone hivi vikiruka hewani mtu anapopiga chafya au kukohoa mtu mwingine huweza kuvivuta ndani na hewa anapopumua hivyo huwa ni muhimu kukaa umbali wa mita 1 kutoka kwa mtu anayeumwa
• Soma: Ugonjwa wa Wengu,Chanzo,Dalili pamoja na Matibabu yake
DALILI ZA UGONJWA WA CORONA COVID19 NI ZIPI?
Dalili za ugonjwa wa Corona COVID19 kwa wagonjwa wengi ni homa, uchovu na kikohozi kikavu. Wagonjwa wengine hupata dalili kama misuli kuuma, pua kubana, mafua kutiririka, maumivu ya koo au kuharisha. Dalili hizi huwa ni ndogo na huanza taratibu.
JE UNAWEZA VIPI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA UGONJWA WA CORONA COVID19
- Nawa mikono mara kwa mara kwa maji na sabuni au kutumia dawa maalumu ya kuua wadudu (Hand sanitizer)
Kwa nini? Ukinawa mikono kwa sabuni na maji au kutumia dawa maalumu ya kusafisha mikono utaua virusi ambao hukaa kwenye mikono mara nyingi
- Jiweke mbali zaidi ya mita moja kutoka kwa mtu anayekohoa au kupiga chafya.
Kwa nini? Mtu anapopiga chafya au kukohoa hurusha chembechembe za mate ambazo huweza kuwa zimebeba virusi. Ukiwa karibu sana utawavuta virusi hawa unapovuta hewa kupumua.
- Acha kushikashika macho, pua na mdomo kwa mikono ambayo hujaisafisha
Kwa nini? Mikono hugusa sehemu mbalimbali hivyo huweza kubeba virusi. Unapogusa macho ,pua au mdomo virusi hupata njia ya kuingia mwilini na kukufanya uugue.
- Iwapo unaumwa mafua, homa au shida ya kupumua usiendelee na shughuri zako nenda hospitali
Kwa nini? Vituo vya huduma ya afya vina taaarifa zote kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa corona pia huweza kukupatia tiba sahihi kuhusu tatizo lako pia hukulinda na kusaidia usisambaze maambukizi kwa watu wengine.
.Kutokushikana mikono au kukumbatiana
• Soma: Ugonjwa wa Wengu,Chanzo,Dalili pamoja na Matibabu yake
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!