UGONJWA WA KICHOCHO,VISABABISHI VYAKE,DALILI,VIPIMO,MATIBABU NA MADHARA YAKE
UGONJWA WA KICHOCHO HUSABABISHWA NA NINI?
Huu ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea ambao kwa kitaalam hujulikana kama aina ya SCHISTOSOMA.
MTU HUAMBUKIZWAJE?
Ugonjwa huu huambikizwa kupitia maji yenye vimelea hivi vya SCHISTOSOMA vinapopenya kwenye Ngozi ya mtu.
DALILI ZA UGONJWA WA KICHOCHO
- Kupata maumivu makali ya Tumbo
- Kujisaidia kinyesi chepesi kilichochanganyika na Damu
- Kukojoa Damu wakati wa haja ndogo
- Kupatwa na hali ya kikihozi
- Kupata Homa
- Kuanza kuwashwa sana na Ngozi
- Pamoja na mwili kuchoka kupita kiasi
VIPIMO VYA KICHOCHO NI PAMOJA NA
- kipimo cha Damu
- Kipimo cha Mkojo
- Kupigwa X-ray ya tumbo
- Au kupigwa Ultrasound ya Tumbo
MATIBABU YA UGONJWA WA KICHOCHO
Ugonjwa huu hutibika kupitia Dawa aina ya PRAZIQUANTEL ambapo mgonjwa atapewa Dose moja tu,hilo tatizo litaisha.
MADHARA YA UGONJWA WA KICHOCHO
Ni pamoja na kupatwa na Magonjwa ya Figo pamoja na Saratani ya Kibofu cha Mkojo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!