UGONJWA WA KIHARUSI NINI?HUSABABISHWA NA NINI?DALILI ZAKE NA TIBA YAKE

Kiharusi ni tatizo linalotokea baada ya kukoma kwa usafirishwaji wa damu kwenye ubongo hivyo kufanya seli za eneo husika zianze kufa kwa mamia. Kiharusi kinaweza kuwa cha aina mbili ambazo ni kile kinachotokea baada ya kuziba kwa mirija inayosafirisha damu kwenye ubongo au pia aina ya pili ni ile inayotokea baada ya kuvujia kwa damu kwenye ubongo


Kiharusi huathiri mwili mzima,au upande fulani wa mwili kutokana na aina ya eneo la ubongo lililoumizwa na ukosefu wa damu,hewa na virutubisho.Kwa lugha rahisi kabisa,pamoja na athari zingine kubwa kiafya,kiharusi husababisha kupooza kwa mwili


Kanuni ya “Act FAST” hutumika kuwatambua na kuwasaidia wagonjwa wa kiharusi. Kwa kuwa familia zetu zinao wagonjwa wanaosumbuliwa na matatizo mengi ya kiafya ambayo yanaweza kupelekea kutokea kwa tatizo la kiharusi ni vyema tukaijua kanuni hii ambayo hufanya kazi kama ifuatavyo

F-FACE (Uso): Misuli ya uso huanza kudondoka,midomo huenda upande (hupinda)

-

A-ARMS (Mikono): Mikono hukosa nguvu za kunyanyuliwa juu,mwelekeze mgonjwa anyanyue mikono yake miwili juu. Watu hawa hushindwa kuinyanyua,hata ikifanikiwa kunyanyuka hudondoka tena baada ya sekunde chache tu

-

S-SPEECH (Mazungumzo): Huanza kupata ugumu katika kuzungumza ama kwa kutokuweza kabisa kufungua midomo au kwa kuzungumza vitu visivyoeleweka. Tambua dalili hii kwa kuzungumza jambo fulani kisha mwambie arudie kama ulivyozungumza

-

T-TIME (MUDA): Muda ndiyo kila kitu,saa pekee ya kumuokoa mtu husika ni muda huohuo. Mfikishe hospitalini mapema,kinyume cha hapo inaweza kuwa changamoto kubwa (kwake na familia)


Haya ndiyo mambo makuu manne ya kuzingatia. Kuna dalili zingine nyingi sana za tatizo hili zinazofanana na magonjwa mengine tu,lakini zilizowekwa hapa ni maalumu kwa kiharusi. Unaweza kuzifuatilia pia pamoja na hizi zilizotajwa hapa ili kusaidia katika jukumu la kuokoa uhai. cc.afyainfo 

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!