UGONJWA WA MONKEYPOX
Imeandaliwa na @doktamathew
Huu ni ugonjwa wa kuambukizwa unaofanana kila kitu na ugonjwa wa ndui(smallpox). Ni ugonjwa ambao umekua changamoto kubwa sana kwani inakua sio rahisi kujua kama ni ndui,surua tetekuwanga nk na kwa maana hiyo kirusi huyu anaweza kutumika kama silaya ya kibaolojia kwenye masuala ya kigaidi(bioterrorism).
Ugonjwa huu ilugundulika miaka ya 1950 nchini DR congo na uligundulika katika makundi ya tumbili(monkey) ambao walikua wagonjwa
Mgonjwa huupata ugonjwa huu kutokana na kugusana na majimaji ya aina yeyote kutoka kwa mnyama mgonjwa au kung’atwa na mnyama mgonjwa,mtu mwenye ugonjwa huu anaweza kumuambukiza mtu mwingine kupitia kugusana na hata kwa njia ya hewa kama anapiga chafya au kukohoa
DALILI
Dalili za ugonjwa huu ni kama za ndui kama nilivosema hapo juu; mara mtu aambukizwapo ugonjwa huu dalili zinaweza kuonekana kati ya siku 5 hadi 21
Mojawapo ya dalili ni kama ifuatavyo
1) Upele upele na harara(rash)-hii ndo dalili ya kwanza kabisa kuonekana
2) Kupata joto kali(fever)
3) kuchoka choka mwili(malaise)
4) Maumivu ya kichwa(headache)
5) Kuvimba mitoki(lymphadenopathy)
6) Maumivu ya misuli(myalgia)
7) Maumivu ya viungo(anthralgia)
8) Kutetemeka tetemeka hata kama una joto kali(chills/shivering)
MATIBABU
Matibabu ya ugonjwa huu mara nyingi hua ni ya kumsaidia mgonjwa kutokana na namna alivokuja(supportive management),mara nyingi watu wengi hupona kabisa kutoka kweye ugonjwa huu;kama hali ya mgonjwa haitakaa vizuri basi zipo dawa maalumu mgonjwa itabidi apewe ili kumsaidia. Habari nzuri ni kwamba ugonjwa huu hauui sana kama ilivyo magonjwa mengine.
NAMNA YA KUJILINDA NA UGONJWA HUU
Kujilinda na ugonjwa huu unatakiwa upate chanjo ya ndui kama upo katika maeneo hatarishi au umekutana na mgonjwa mwenye dalili za ugonjwa huu au umekutana na mnyama wa jamii ya tumbili anaeumwa.
#doktamathew
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!