UGONJWA WA POLIO AFRIKA

POLIO

• • • • • •

Afrika imetangazwa kuumaliza ugonjwa wa polio na Shirika la Afya Duniani pamoja na Tume ya Ukanda wa Afrika ya kupambana na Polio.


Polio huathiri watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, wakati mwingine husababisha kupooza. Kifo kinaweza kutokea iwapo kupooza huko kutaathiri misuli inayosaidia mfumo wa upumuaji.


Hakuna tiba lakini chanjo dhidi ya ugonjwa huo huwalinda maisha yao yote. Ugonjwa huo sasa uko Afghanistan na Pakistan pekee.


Nigeria ni nchi ya mwisho kutangazwa kuutokomeza ugonjwa huo mbaya, ikiwa na wagonjwa zaidi ya nusu ya wagonjwa wote wa polio duniani chini ya miaka kumi iliyopita


Pongezi nyingi kwa wahudumu wa afya na asasi zote zilizowezesha mafanikio haya

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!