UGONJWA WA TEZI DUME
Kila mwanaume anazaliwa na Tezi ya kiume. Tezi dume siyo ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini. Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo. Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani; na husaidia mbegu za kiume kubaki hai kwa muda unaostahili.
Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu mnoo. Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi.
Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 5 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.
UKUAJI WA TEZI DUME
Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.
Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa miaka zaidi ya 50.
Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume, mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; Na 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume.
Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.
• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo
VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA
Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi. Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jami kuhusu afya bora na Virutubisho.
Vifuatavyo ni vyanzo vya kutanuka kwa tezi dume:
- Ukosefu wa lishe kamili na upungufu wa Virutubisho muhimu mwilini
- Uwepo wa sumu nyingi na mafuta mengi mwilini hasa katika mishipa na ogani za uzazi
- Kutokufanya mazoezi
- Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara
- Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi
- Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance)
- Msongo wa mawazo (Stress )
- Magonjwa ya zinaa
- Umri mkubwa
- Upasuwaji wa korodani,matatizo ya kimaumbile ya Korodani
- Historia ya Familia (Kurithi)
- Mazingira (Ethnicity
DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME
Tatizo la Tezi Dume si tatizo la kutokea tuu siku moja na mara moja tuu. Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), atambue alianza kupata tatizo hilo kwa muda mrefu sana, Wengi wao hueleza dalili za tatizo hili huanza kuziona si chini ya miaka 3.
Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa, ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer). Saratani ziko stage nne.
Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki. Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.
Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako
mzima wa uzazi wa mwanaume.
a) Dalili za awali - Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
- Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
- Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
- Homa
- Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
b) Dalili za mtu aliyeathirika - Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
- Miguu kuwa dhaifu
- Kushindwa kumudu tendo la ndoa, au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
- Kushindwa kuzuia mkojo , pindi unapohisi kukojoa
- Kushindwa kuzuia haja kubwa
(kinyesi cha maji maji)
- Tumbo kujaa gesi mara kwa mara
• Soma: Tatizo la Mapunye Kichwani kwa Watoto wadogo
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
UGONJWA WA TEZI DUME(SARATANI YA TEZI DUME),CHANZO,DALILI,VIPIMO NA TIBA YAKE
Moja ya matatizo yanayoathiri aina ya Tezi linalojulikana kama tezi dume ni saratani ya tezi dume. Saratani ya tezi dume huchukua nafasi ya tatu katika kusababisha vifo kwa wanaume wenye umri mbalimbali duniani. Lakini pia Ugonjwa huu ni chanzo kikubwa cha vifo kwa wanaume wenye umri wa miaka 70 na kuendelea. Hata hivyo, ni nadra sana kwa saratani ya Tezi Dume kuwapata wanaume chini ya miaka 40.
📶 WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATA SARATANI YA TEZI DUME
- Wanaume ambao asili yao ni Afrika wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa Saratani ya tezi Dume ikilinganishwa na wazungu
- Wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea
- Wanaume ambao wana historia ya tatizo la Saratani ya Tezi Dume katika familia zao, Mfano, wale ambao mmoja wa ndugu zake (kaka au mdogo wa kiume) au baba amewahi kuugua ugonjwa huu.
- Wanaume walevi au wanaokunywa pombe kupindukia
- Wanaume Wanaofanya kazi kwenye viwanda mbali mbali hasa vya kutengeneza rangi au wanaofanya kazi ya kupaka rangi
- Wanaume ambao ni Wakulima wanaotumia aina fulani ya mbolea zenye kemikali
- Wanaume Wanaofanya kazi katika viwanda vya utengenezaji matairi
- Wanaume wanaofanya kazi ya kuchimba madini hususani aina ya cadmium
- Wanaume wanaokula chakula chenye kiasi kikubwa cha mafuta hasa ya wanyama
🔻DALILI ZA UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME
-Tafiti zinaonyesha kwamba saratani ya Tezi Dume ikiwa katika stage au hatua za mwanzoni, dalili zake hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume (BPH). Dalili hizo ni pamoja na;
- Mwanaume Kupata maumivu au kuteseka wakati wa kukojoa
- Mwanaume kupatwa na hali ya kutiririka kwa mkojo baada ya kumaliza kukojoa
- Mwanaume kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
- Mwanaume kukojoa mara kwa mara hasa nyakati za usiku
- Mwanaume kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote
- Mwanaume kutoa mkojo uliochanganyika na damu
- Mwanaume kutoa mbegu za kiume( shahawa) zilizochanganyika na damu
Endapo Ugonjwa huu wa Saratani ya Tezi dume umesambaa kwa kiasi kikubwa,Mgonjwa ataonyesha dalili zifuatazo;
➖ Mwanaume kupata Maumivu makali ya mifupa katika maeneo ya nyonga, mapajani na kiunoni
➖ Hali ya Uume kushindwa kusimama (uhanithi)
➖ Pia mwanaume mwenye tatizo la Saratani ya Tezi dume huweza kupata dalili Za jumla kama vile;uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu, kizunguzungu n.k
🔴 VIPIMO CHA TATIZO LA TEZI DUME
Ili kuweza kutambua tatizo la saratani ya tezi dume kuna mambo mbali mbali hufanyika kama vile;
* Kutaka kujua historia ya magonjwa mbali mbali katika familia husika,ikiwemo historia ya tatizo hili la Saratani ya Tezi Dume
*kutaka kufahamu kuhusu dalili mbali mbali anazopata Mgonjwa au zinazojionyesha kwa Mgonjwa
*Ufanyaji wa Vipimo mbali mbali kama vile;
- Digital rectal exam: Hapa mtaalam wa afya au Daktari ataingiza kidole cha shahada katika puru (rectum) ili kuhisi tezi dume kupitia ukuta wa puru. Aidha atahisi pia sehemu zote zinazozunguka tezi dume kutambua iwapo tezi ni ngumu au kama ina uvimbe wowote.
- Kuna kipimo cha damu kuchunguza Prostate Specific Antigen (PSA): PSA ni aina ya protein inayozalishwa na seli za tezi dume. Uzalishaji wake huongezeka wakati wa BPH, tezi dume inapopata uambukizi (prostitis) , na saratani ya tezi dume.
- DRE pamoja na PSA huonesha uwepo wa tatizo kwenye tezi dume lakini vipimo hivi havina uwezo wa kutofautisha iwapo tatizo hilo linamaanisha saratani au BPH. Hivyo basi, ili kuweza kutofautisha kati ya magonjwa hayo mawili, kipimo kiitwacho Prostate biopsy hufanywa.
- Prostate biopsy: Kipimo hiki hufanywa kwa kuchukua kipande cha nyama (tishu) kutoka tezi dume kwa ajili ya uchunguzi maabara.
- Kipimo kingine huitwa transrectal ultrasound ambacho husaidia kuonesha ukubwa na sura ya tezi dume lilivyo.
☑️ MATIBABU YA SARATANI YA TEZI DUME
Matibabu ya Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume ni pamoja na;
- Mgonjwa kufanyiwa upasuaji na tiba ya mionzi,
-Lakini kwa wagonjwa wazee, kuendelea kufatiliwa kwa ukaribu zaidi pasipo kufanyiwa upasuaji au tiba yoyote inayohisu mionzi.
-Endapo saratani imesambaa kwa kiasi kikubwa na kuathiri sehemu nyingine za mwili, matibabu yake yanaweza kujumuisha upasuaji wa kuondoa korodani, matumizi ya dawa za kupunguza kiwango cha homoni ya testosterone katika damu (hormonal therapy), au matumizi ya kemikali za kuua seli za saratani (chemotherapy).
- Tiba ya miozi huweza kutumika Kwa wagonjwa walio katika hatua ya mwisho ya saratani yaani wale ambao saratani tayari imeshasambaa mwilini ili kupunguza maumivu makali ya mifupa.
👉 Lakini Madhara ya tiba hii ya mionzi ni pamoja na mwanaume kushindwa kusimamisha uume au uhanithi, kukosa hamu ya kula, uchovu, ngozi kubabuka, kuharisha na kutoa mkojo uliochanganyika na damu.
- Matibabu yanayohusu homoni
Aina hii ya tiba inahusu matumizi ya dawa zinazopunguza kiwango au ufanyakazi wa homoni ya testosterone mwilini. Testosterone ni homoni ya kiume inayochochea ukuaji wa tezi dume, hivyo basi matumizi ya dawa hizi husaidia kupunguza ukuaji pamoja na kusambaa kwa seli za saratani.
👉 Lakini pia,Madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya dawa hizi ni pamoja na kichefuchefu na kutapika, upungufu wa damu, kuongezeka uzito, uhanithi na kukosa hamu ya tendo la ndoa,matatizo katika ini na matiti kuwa makubwa.
KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!