UJUE UKWELI KUHUSU LIMAO NA KUPUNGUZA DAMU
• • • • • •
Tumekuwa tunasikia tangu zamani (mtaani) kuwa ulaji mwingi wa limao au ndimu hupunguza damu. Jambo hili siyo kweli
-
Limao/ndimu huwa na faida ya kuongeza uzalishwaji wa damu,hasa chembechembe nyeupe za damu zinazosaidia kuulinda mwili na kuongeza kinga yake (Askari wa mwili). Hushusha presha,hupunguza nafasi ya kuugua kiharusi,hutoa kinga dhidi ya aina mbalimbali za saratani,husaidia katika kupunguza uzito uliozidi,huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula pamoja na kuboresha mfumo wa upumuaji.
-
Miongoni mwa faida zingine za limao/ndimu ni kusaidia kuharibu sumu za mwili hasa kwa watu wanaolewa pombe na wavutaji wa sigara. Hii ndiyo sababu inayowafanya watu wanaovuta sigara na kulewa pombe kali wahitaji kiasi kikubwa zaidi (yaani 35 mg za ziada ) cha vitamin C kila siku kuliko watu wengine,na wanaweza kuzipata kwa uhakika kupitia tunda hili kwa mfumo wa juisi yake,au hata kwa kulamba maji yake
-
Limao/ndimu husaidia katika kuzuia tatizo la anemia,ambalo kwa lugha rahisi kabisa hutokana na kupungua kwa mzunguko wa chembechembe nyekundu za damu kwenye mfumo mzima wa damu mwilini. Kwa mujibu wa takwimu za jarida la kitabibu la The Lancet,moja ya tatu ya watu wote tunaoishi duniani tunakabiliwa na aina mojawapo ya anemia mwilini. Matumizi ya tunda hili huongeza ufyonzwaji wa madini ya chuma ambayo ni muhimu sana katika utengenezwaji wa damu hivyo kukuepusha dhidi ya tatizo hili
-
Dalili chache za anemia ni kama vile kupauka kwa rangi ya ngozi,kupumua harakaharaka bila uwepo wa kazi yoyote ngumu,kubadilika mara kwa mara kwa utaratibu wa kawaida wa mapigo ya moyo,kukata kwa pumzi,uchovu bila sababu,maumivu ya kifua pamoja na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara cc.afyainfo
.
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!