UMUHIMU WA KULA MAPERA MWILINI
MAPERA
• • • • • •
Mapera yana faida nyingi mwilini kwani husaidia kuweka uwiano sahihi wa madini ya sodiamu na potasiamu katika mwili, hivyo kuweka sawa shinikizo la damu. Pia hupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuepusha maradhi ya moyo.
Mapera pia huwa na uwezo wa kudhibiti sukari mwilini na tafiti kadhaa zimeonesha kuwa juisi ya mapera kwa watu wenye matatizo ya sukari imekuwa ikileta matokeo chanya
Pia huwa na Vitamin C nyingi inayowezesha kuimarisha kinga ya mwili. Vilevile mapera huwa na protini ya kutosha ambayo huhitajika na mwili ili kuujenga mwili.
Mapera yameonekana kupunguza dalili za maumivu nyakati za hedhi haswa maumivu ya tumbo. Pia, mapera ni chanzo cha nyuzinyuzi (fiber) ambazo hi muhimu kwa ajili ya mmeng'enyo wa chakula.
Mapera pia huimarisha afya ya ngozi kwa kuwa huwa na 'antioxidants' za kutosha ambazo ni muhimu katika kuepusha ngozi kuweka haraka. Na pia, pera likiwekwa moja kwa moja juu ya chunusi huweza kuleta matokeo chanya.
Jitahidi kula mapera kwani huwa na Faida nyingi mno mwilini
#drtareeq
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!