UMUHIMU WA KUNYWA MAJI MWILINI
KUNYWA MAJI KWA AFYA YAKO
Maji huchukua takribani asilimia 75% ya Mwili wote wa Binadamu. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi wamechukulia umuhimu zaidi wa Chakula kuliko Maji. yajue maajabu haya ya Maji katika Mwili wako
• • • • • •
1. Usipokunywa maji utakufa haraka
Kwa ufupi, ni dhahiri kuwa usipokunywa maji utakufa. Maji ni muhimu zaidi kwenye mwili wa binadamu hata kuliko chakula. Ni dhahiri kwamba sipokula chakula utakufa, lakini utakufa ndani ya siku chache zaidi kama hautakunywa maji.
2. Huzuia Saratani
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa watu wenye tabia za kunywa maji mengi kadri inavyotakiwa (angalau lita 3 kwa siku) wana nafasi nzuri zaidi ya kupunguza uwezekano wa kupata saratani kwa asilimia 45.
3. Hupunguza msongo wa mawazo
Tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ukosefu wa maji ya kutosha mwilini kunaweza kuathiri uwezo wa kufikiria wa binadamu na kumfanya aweze kuchanganyikiwa na mambo kwa uharaka zaidi kuliko mtu ambaye anakunywa maji mengi. Mtu anayekunjwa maji mengi huwa na uwezo mzuri wa kufikiria kwa utulivu na kuikaribisha furaha zaidi.
Ukiwa na msongo wa mawazo, utakuwa katika wakati mgumu zaidi endapo utakuwa haunywi maji mengi kwa kuwa uwezo wako wa kufikiria umeathiriwa na ukosefu wa maji.
#afyasolution
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!