USUBIRI MUDA GANI UNAPOKUWA ULIJIFUNGUA KWA UPASUAJI ILI UBEBE TENA MIMBA NYINGINE

🔻USUBIRI MUDA GANI UNAPOKUWA ULIJIFUNGUA KWA UPASUAJI ILI UBEBE TENA MIMBA NYINGINE

Happy NEW YEAR 2021 my Lovely followers.

Kwanza kabisa nianze mwaka kwa Kusema NAWAPENDA SANA,na NAWATHAMIN SANA.

Naona NIANZE NA hili,Hakuna swala ninapigia kelele na kushauri mara kwa Mara Kama hili 

Ili kupunguza VIFO vya mama na mtoto,HILI ni Muhimu kuzingatia.

Mama haujalishi mtoto Yupo hai au bahati mbaya Mungu kamchukua(Polen sana mnaopitia hili,Nimeshuhudia na wengi wanapitia Hili,Mungu awape Faraja,na Awajaalie tena Mje mpate Hii BARAKA) ,muda wa kusuburi Kwa usalama Wa MAMA ni Ule ule,Unatakiwa UKAE MIAKA miwili  au ZAID ndipo Upate mimba(Unapokaa miaka mingi ZAID yaan MINNE,MITANO ni salama ZAID).

HASARA za kubeba MIMBA kabla ya MUDA; unakuwa hatarini KUCHANIKA KIZAZI maana mshono wa zaman ni Rahis Kuchanika mama  anapopota uchungu tu(na wengine mshono kwa kizazi unaachia bila Hata uchungu kwa wenye mshono zaid ya mmoja hii ni hatar zaid,tunaita SILENT RUPTURE).

Na kizazi kikichanika,mwanamke huyu hupoteza damu sana na  UHAI/MAISHA yanakuwa hatarin na Tumepoteza wanawake Wengi kwa HILI.


Wanawake wa kwenye Jamii,unakuta MNASHUHUDIA  TU na Kuona TU wamama WANAOPATA MIMBA MSHONO UNA MIEZI 10,au MWAKA MMOJA,wanajifungua salama kabisa,Sisi watumishi wa Afya tunakutana na Wanawake wanaochanika vizazi KWA KUBEBA MIMBA juu ya mishono mibichi.


Let us CHANGE,umeambiwa Miaka Miwili,au MITATU,VUMILIA,BE PATIENT,mwombe MUNGU,Muda ukifika Inshaalah UTABARIKIWA utaitwa MAMA.


Wanawake,wamama,FUATEN USHAURI TUNAOWAPATIA,achanane na ushauri wa Mtaani.


Mtu kasema analeta Hoja mezan anakuambia Mama X anabeba mimba mtoto hata MWAKA hajafunga,kwa hiyo NAE ANATAKA ABEBE MIMBA.


Kila mtu na UZAZI WAKE,Na ni jinsi Upasuaji wake ULIVYOKUWA,walivyoshona kizazi chake.

Mliofanikiwa Mshukurun MUNGU kawapitisha SALAMA,Msiwe chachu kufanya wengine WAIGE.


N:B chanzo cha VIFO vitokanavyo na UZAZI sababu ya KWANZA ni wanawake Kumwaga Damu sana,Sasa katika vyanzo vya kumwaga damu,Kuchanika kizazi Ni moja wapo.

@uzazipoint @uzazipoint @women


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!