Ticker

6/recent/ticker-posts

UTE UNAOASHIRIA SIKU ZA HATARI YA KUPATA MIMBA



UTE

• • • • • •

UTE UNAOASHIRIA SIKU ZA HATARI YA KUPATA MIMBA


Hormone zinazochochea  mayai kutengenezwa ndo hizo hizo zinachochea kutengenezwa,kwa ute unaosaidia mbegu za kiume zijongee vizuri.


Hormone ya estrogen ndo inahusika na hili. Endapo una estrogen kidogo huwez pata ute au kama mfumo wa estrogen na progesterone haujakaa katika uwiano mzuri huwezi pata ute.


Ute unaovutika huanza kutokea siku chache kabla ya yai kuachiliwa. Japo wengine wenye tatizo la Polycystic ovarian syndrome wanakua wanapata ute huu zaidi ya mara moja katika mizunguko yao.


Ute huu unapozalishwa unaambata na joto kupanda. Kama unapata ute na joto hakuna mabadiliko bas inaweza kua yafatayo

1.haupevushi mayai

2.hau chart vizuri


JINSI YA KUANGALIA UTE

1.nawa mikono

2.weka kidole cha kati ukeni ndani. Kama unatoa ute mwingi basi haina haja ya kuingia ndani

3.toa kidole na kuangalia ute ukoje






Post a Comment

0 Comments