UZITO WA MTOTO KATIKA UKUAJI WAKE
Moja ya vitu ambavyo huangaliwa sana katika maendeleo ya mtoto au Ukuaji wake ni pamoja na Uzito wake. Tangia tu mtoto kuzaliwa pale hadi anavyoendelea na ukuaji wake,bado uzito wake huendelea kufwatiliwa kwa ukaribu sana.
Uzito wa mtoto hufwatiliwa baada ya kuzaliwa na kipindi chote cha kliniki yake,lengo likiwa ni kuchunguza ukuaji wake pamoja na maendeleo ya afya yake.
Wastani wa Uzito wa kawaida kwa mtoto kuzaliwa ni Kilogram 2.5 mpaka 3.5, hivo basi mtoto akizaliwa na zaidi ya kilogram 3.5 tunasema mtoto huyu kazaliwa na uzito mkubwa au tunaita BIG BABY(MTOTO MKUBWA), Lakini pia mtoto akizaliwa na uzito wa chini ya kilogram 2, huyu naye tunamuweka katika kundi la watoto waliozaliwa na uzito mdogo sana,na wanaohitaji uangalizi wa karibu sana, kwani uzito wa mtoto huangalia pia na afya yake.
Je wewe mtoto wako alizaliwa na kilogram ngapi?
Katika kipindi cha kliniki kuanzia mtoto anapoanza mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano,Pia uzito wake huendelea kuchunguzwa kwa ukaribu, na kama uzito wake hauendani na ukuaji wake,au umri wake,jitihada mbali mbali hufanyika ikiwa ni pamoja na mama kushauriwa kwa kina juu ya lishe ya mtoto.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!