VIDOKEZO 15 VINAVYOHUSU UGONJWA WA UTI

UTI

• • • • • •

1.Kunywa maji kwa wingi kila siku


2.Epuka tabia ya kubana mkojo kwa muda mrefu


3.Wanawake wanapaswa kubadili pedi mara kwa mara wakati wanapokuwa katika hedhi, angalau wabadili pedi mara 2-3 kwa siku.


4.Epuka kujisafisha ukeni kwa sabuni zenye kemikali, pia kupulizia marashi


5.Pale unapojisafisha baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia kwenye njia ya mkojo.


6.Boresha usafi wa vyooni, mwaga maji kabla ya kwenda haja ndogo na tumia maji safi na salama kujisafisha sehemu za siri. 


7.Epuka kujamiiana kinyume na maumbile kwani chanzo cha U.T.I ni bakteria wapatikanao njia ya haja kubwa.


8.Safisha uke kabla ya kushiriki tendo la ndoa na nenda haja ndogo baada ya kumaliza kujamiiana


9.Tumia mipira ya kujikinga yenye vilainishi au mafuta ili kupunguza kutokea kwa michubuko ukeni ambayo uwepo wake ni mazalia ya vimelea.


10.Vifaa vya kupanga uzazi kama vile diaphram, kondomu kavu na mafuta mazito ya kuangamiza mbegu za kiume huambatana na michubuko. Hakikisha unatumia vifaa hivi katika viwango sahihi.


11.Kausha maeneo ya ukeni kwa kitambaa safi na kikavu, vaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba ili zisaidie kunyonya majimaji kirahisi


12.Vaa nguo za ndani zisizobana mwili, epuka kuvaa nguo ngumu zinazobana mwili na nguo za ndani zilizotengenezwa kwa nailoni au silk


13.Kula lishe bora na kuzingatia kanuni za afya ikiwamo mlo uliosheheni protini, mboga za majani na matunda ili kujenga kinga imara ya mwili.


14.Pale unapopata dalili au viashiria vya awali fika mapema katika huduma za afya zinazotambulika na serikali kwa ajili ya uchunguzi, matibabu na ushauri.


15.Epuka matibabu yanayotolewa kienyeji mtaani na watu wasio na sifa stahiki za kutoa matibabu ya binadamu. Zingatia matibabu ya wataalam wa afya na usikatishe dozi.

Via Dr.tareeq


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!