MIMBA
• • • • • •
VISABABISHI NA DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA
Mimba inapoharibika yenyewe kabla ya kutimia umri wa wiki 20 hujulikana kama miscarriage. (kuharibika kwa mimba).
Karibia 50% ya mimba zinazoharibika huharibika bila wanawake kujua kama walikuwa wajawazito. Huenda unahangaika kutafuta ujauzito ila kumbe huwa unapata ujauzoto na unatoka bila wewe kujua.
Zipo sababu nyingi za kuharibika kwa mimba baadhi ya sababu hizo ni kama vile:
➢ Kukosekana kwa uwiano wa vichocheo (Hormonal imbalance) ambavyo ni muhimu sana katika ukuaji wa mimba.
➢ Matatizo katika maumbile ya mfuko wa uzazi
➢ Uvimbe katika mfuko wa kizazi (Fibroids au mayoma)
➢ Kulegea kwa shingo ya kizazi.
➢ Ulevi
➢ Matumizi ya dawa kiholela kipindi cha ujauzito pasipo maelekezo ya daktari
➢ Uzito uliopitiliza
➢ Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari, ugonjwa wa shinikizo la damu
➢ Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke
➢ Matatizo kwenye shingo ya kizazi
➢ Kuwepo kwa kifafa cha mimba
Dalili za kuharibika mimba
➢ Kutokwa damu kwenye njia ya uzazi ya mwanamke ambapo huanza kama matone na baadae kuongezeka kuwa nyingi
➢ Maumivu makali ya chini ya kitovu, kiuno na mgongo
➢ Kutohisi mtoto akicheza ndani ya tumbo la mama mjamzito
➢ Hali ya homa na uchovu
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!