VYANZO VYA VIFO VYA GAFLA KWA WATOTO

VIFO KWA WATOTO

• • • • • •

Ni vifo vya ghafla visivyoelezeka, mara nyingi vichanga vikiwa vimelala, huwakumba vichanga vyenye afya imara tu. Haswa, watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja.


CHANZO

Sababu kuu haifahamiki lakini huhusishwa na tabia hatarishi mbalimbali, kama zifuatazo;


VIHATARISHI 

1. Matatizo katika ubongo yanayohusika na upumuaji nyakati za kulala

2. Uzito mdogo wa kuzaliwa (huweza kupelekea matatizo katika ubongo)

3. Maambukizi katika njia ya hewa 

4. Kumlaza mtoto kwa tumbo ama upande. Baadhi ya watoto hushindwa kupumua vizuri katika ulalaji huu tofauti na kulala chali

5. Kulazwa kitanda kimoja na wazazi au watu wengine kwani wanaweza kubanwa pumzi

6. Joto kali

7. Jinsia ya kiume, japo wa kike pia hupatwa na shida hii

8. Vichanga vyenye umri kati ya miezi 2-3 huathirika zaidi

9. Vichanga Weusi (wenye asili ya Afrika huathirika zaidi) 

10. Historia ya tatizo hilo katika familia 

11. Wazazi wanaovuta sigara


NAMNA YA KUMKINGA MTOTO

1. Usijaze vitu kitandani kwa mtoto

2. Usivute sigara mbele ya mtoto wako

3. Usilale na mtoto kitanda kimoja kama haiwezekani kuwa makini ukilala naye usimbane pumzi

4. Mnyonyeshe mtoto mara nyingi uwezavyo

5. Hakikisha mwanao anapatiwa chanjo zote kwa wakati 

6. Usimvishe nguo nyingi mtoto kipindi cha joto

7. Usimlishe mtoto wa chini ya mwaka mmoja asali. Asali huweza kusababisha BOTULISM (usumu kutokana na Clostridium botulinum bakteria kutoka katika asali). Hali hii inahusishwa na SIDS

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!