HEDHI
• • • • • •
WAKATI WA HEDHI KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI.
Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili;
Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
SABABU INAYOPELEKEA MAUMIVU. -kutofanya mazoezi.
-Kutokula matunda kwa wingi.
-Kutokula mboga za majani
-Pia ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa wingi, mfano Chipsi.
Sasa leo nakujuza vyakula vichache endapo utapendelea kuvitumia basi utamaliza au kupunguza kwa kiasi kikubwa maumivu hayo.
PAPAI BICHI;
Papai lina uwezo mkubwa wa kulainisha misuli ya mirija ya uzazi hivyo kurahisisha utokaji wa hedhi bila maumivu.
Tunda hili lina manufaa zaidi kwa wasichana hasa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na stress. Utapata faida hizo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi(halijaiva ila limekomaa)
UFUTA;
Jinsi unavyoweza kuandaa ufuta kwa tiba ya maumivu wakati wa hedhi ni kusaga ufuta na upate unga wake kisha changanya na maji ya moto. Kunywa mara mbili kwa siku.
Tiba hii huwafaa zaidi wasichana wadogo au wanawake wanaotoka hedhi kidogo zaidi
TANGAWIZI;
Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na uweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo kwa siku mara mbili baada ya mlo.
Tutaendelea kuelezea zaidi vyakula vingine, .
.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!