WANAWAKE KULALA CHALI WAKATI WA UJAUZITO.
Wanawake wajawazito wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kupata matatizo mbali mbali kutokana na kubonyeza mshipa mkubwa unaojulikana kama INFERIOR VENA CAVA. Matatizo hayo ni pamoja na kupata maumivu makali ya nyongana tumbo,miguu kuvimba,presha kushuka, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo na kuzaa mtoto mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi. Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine walizaa watoto wafu.
Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000 wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu. Hata hivyo, utafiti mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto wafu wanaozaliwa katika nchi zenye raia wenye kipato kikubwa
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!