WANAWAKE KUSUMBULIWA NA MATATIZO YA MIFUPA KULIKO WANAUME
Uwepo wa Matatizo ya Mifupa Kwa Wanawake zaidi ya Wanaume
• • • • • •
Wanawake wanakabiriwa na changamoto ya kupungua kwa ujazo wa mifupa mara nne zaidi kuliko wanaume kadri umri wa kuishi unavyoongezeka. Hii huwafanya wakabiliwe na matatizo makubwa sana ya viungo vya mwili hasa nyonga,mgongo,magoti pamoja na kuvunjika kwa mifupa. Vichocheo vya Estrogen ndivyo huimarisha afya ya mifupa kwa wanawake hivyo wakifikia umri wa ukomo wa hedhi vifuko vyao vya mayai,pamoja na kukoma kutoa mayai kila mwezi hupitia pia changamoto za kuzalisha kiasi kidogo sana cha vichocheo hivi,au hata kutokuzalisha kabisa
-
Hali hii hudhoofisha sana afya ya mifupa. Kwa wanaume,hali hii huwepo pia japo siyo kwa kiasi kikubwa sana kama ilivyo kwa wanawake. Vichocheo vya kiume vya testosterone,vitamin D,madini ya calcium,ukosefu wa mazoezi pamoja na changamoto zingine pia za kiafya huchangia kwa kiasi kikubwa sana kutokea kwa hali hii.
-
Ili wazee wetu (wake kwa waume) waweze kapunguza tatizo hili,au hata kulishinda kabisa ni lazima washiriki kazi (mazoezi) ya kurudisha utimamu wa miili yao,wapunguze matumizi ya pombe na sigara pia wahakikishe wanatumia vyakula au virutubisho vyenye wingi wa madini ya calcium hasa maziwa na bidhaa zake,soya,mboga za majani pamoja na samaki. Vitamin D hupatikana kwenye mwanga wa jua la asubuhi linalochomoza,samaki na mafuta yake pamoja na virutubisho mbalimbali.Cr.afyainfo
#afyaclass
.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!