WANAWAKE WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UTI

SOMA UGONJWA WA UTI PAMOJA NA WANAWAKE WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UTI

➡️ UTI


UTI KWA WANAWAKE

Kama nlivosema hapo awali kwamba UTI inajumuisha maambukizi kwenye njia ya mkojo(urethritis),kibofu cha mkojo(cystitis) au kushambulia figo zenyewe (pyelonephritis). UTI kwa wanawake huanza kwa staili hii ,kwanza kunakua na uzamiaji Wa bakteria(colonization) ambao Mara nyingi hukaa maeneo ya njia ya haja kubwa na Jirani yake kuzamia kwenye mlango Wa uke(introitus),wakishakaa hapo wanaanza kupanda kidogo na kuingia kwenye njia ya mkojo na hatimae kupanda hadi kwenye figo endapo hutatibiwa mapema.

UTI inaeza kusababishwa na vimelea wa aina mbalimbali wakiwemo bakteria kama Escherichia coli  klebsiella, Proteus, Enterobacter,  Citrobacter,Staphylococcus saprophyticus, Enterococcus na Staphylococcus aureus ,minyoo,virusi kama adenovirus, enteroviruses, Coxsackieviruses, echoviruses,fangasi kama Aspergillus spp, Cryptococcus neoformans, nk.

Wanawake ndo walio kwenye hatari ya kupata UTI sana ukilinganisha na wanaume na  sababu ambazo zinafanya wanawake ndo wawe wanapata shida zaidi ni kwamba njia yao ya mkojo (urerhra ) ni fupi mno,hawana tezi dume na maeneo yao ya siri yana unyevu unyevu mwingi sana tofauti na wanaume ambao wana njia ndefu ya mkojo,wana tezi dume ambayo inatoa kemikali ambayo inakua kama dawa ya kuua hao vimelea na pia maeneo ya siri ya mwanaume ni makavu Mara zote na mwisho ni ukaribu Wa njia zao za mkojo na maeneo ya njia ya haya kubwa.


WANAWAKE WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UTI 

1. Kama ulishawahi kupata UTI (history of UTI)

2. Waliofanya mapenzi siku za karibuni(recent sexual intercourse),Mara nyingi kuna wanawake ambae muda mchache baada ya kufanya mapenzi hasa wanaojihusisha na mapenzi ya njia ya haja kubwa ambapo hupelekea kuhamisha vimelea kitoka nyuma kuwapeleka mbele.

3. Wanaotumia kondomu zenye dawa ya kuua mbegu za kiume(spermicide-coated condoms)

4. Wanaoweka dawa za kuua mbegu za kiume ukeni(spermicides)

5. Mwenye kisukari(diabetes mellitus)

6. Wanawake wenye mawe kwenye mfumo Wa mkojo(nephrolithiasis)

7. Wanawake wenye magonjwa ya figo(CKD/ESRD)

8. wanawake wenye upungufu Wa kinga mwilili utokanao na mambo mbalimbali kama UKIMWI,kisukari,Ujauzito

Na. Dr. Mathew


.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!