WATOTO MAPACHA OR KWA KITAALAM "TWINS"
WATOTO MAPACHA KWA KITAALAM "TWINS"
Kuna Mapacha wa aina mbili. Pacha wanaofanana (identical twins) na pacha wasiofanana (Fraternal twins). Pacha wanaofanana si rahisi sana kupatikana hivyo asilimia kubwa ya pacha ni wale wasiofanana (fraternal twins). Pacha wanaofanana ama identical twins hutokea pale yai linapogawanyika hasa mwanzoni mwa ujauzito na hawa huishi kwenye mfuko mmoja. Mapacha wasiofanana hutokea pale mayai mawili yanapoachiliwa wakati wa ovulation (Hiki ni kipindi ambacho mwanamke anaweza kupata ujauzito).
Nani anaweza kupata mapacha?
Mtu yoyote anaweza kupata mapacha hata kama hana historia ya mapacha katika familia yake.
.
Lakini sababu hizi zifuatazo zinaweza kuongeza uwezekano wa kupata mapacha;
Historia ya mapacha katika familia hasa upande wa mama,watu ambao kwenye familia zao kuna historia ya mapacha ama wao wenyewe ni pacha wana asilimia kubwa ya kupata mapacha.
Asili,wanawake wa kiafrika ama wakimarekani wana uwezekano mkubwa wa kupata watoto mapacha.
Wanawake warefu na wanene wana uwezekano mkubwa waa kupata watoto mapacha kuliko wale wafupi na wembamba(Research center sources)
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!