OVULATION
• • • • • •
Ovulation (kupevuka kwa yai) ni pale yai moja au zaidi yanaachiwa kutoka kwenye moja ya ovari (mifuko ya mayai) yako. Hii hutokea karibia na mwisho wa muda ambao unaweza kupata ujauzito katikati ya mzunguko wako wa hedhi.
Yai/mayai yaliotolewa hudumu kwa masaa 24.Kama mwanamke hatoi mayai hii inamaana hapitii kipindi cha ovulation (kipindi cha hatari),hivyo hawezi kubeba mimba
👉🏼Kuna wanawake ambao hupata siku zao kama kawaida ila hawatoi mayai
👉🏼Baadhi ya wanawake hutoa mayai lakini hayaja pevuka hivyo kusababisha kushindwa kubeba mimba(immature ovum)
👉🏼Baadhi ya wanawake hawajui lini hupata ovulation kwasababu ya siku zao kubadilika hivyo kusababisha kutokubeba mimba
Ndio maana ni muhimu kupata ovulation kit yako mapema na kufatilia mzunguko wako
Kama unapata siku zako bila kutoa mayai hii inamaana una anovulatory cycle mara nyingi huusiana na wanawake wenye shida ya pcos.
Baadhi ya sababu zinazomfanya mwanamke asitoe mayai
1.mabadiliko ya mwili kuongezeka sana uzito (hii ni moja ya sababu kubwa sana ya ugumba take note ladies) BMI 30 or more au kupungua sana uzito hudhuru hormones
2.kupita kwenye kipindi cha stress
3.Infection maambukizi kwenye mji wa uzazi mpaka kwenye mfuko wa mayai
4.kuwa na tatizo la cyst kwenye mji wa uzazi mirija au ovary cyst zenyewe(PCOS)
5.Saratani ya ovary
6.Baadhi ya ovary cyst mbaya kama DERMOID CYST
7.Kisukari
8.Hormone ya prolactin kuwa juu kusababisha maziwa kutoka kwenye chuchu hata kama sio mama mjamzito (hyperprolactinemia)
9.Mwanamke aliebaki na mayai ma chache kwenye mfuko wake wa mayai (ovary)
10.Mwanamke anae wahi kufika kikomo cha hedhi,premature menopause inayoanza kuanzia miaka 30-35
11.Mwanamke anaeingia kikomo cha hedhi ambacho ni miaka 45-52
Kama una shida katika kupevusha mayai unaweza kupata ovulation kit hii pia inasaidia wanaopenda twins inaweza kusaidia
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!