VIATU VIREFU
• • • • • •
YAJUE MADHARA YA KUVAA VIATU VIREFU (HIGH HEELS)
Mbali na kwamba uvaaji wa Viatu virefu maarufu kama high heels siku hizi umepamba moto,na imeonekana kama Fashion na inaongeza sana Mvuto wa kipekee kwa Mwanamke.Kiafya uvaaji huo sio salama kabsa.
Madhara huweza kuonekana katika maeneo mbali mbali ya Mwili kama vile kwenye KIUNO,MGONGO au UTI WA MGONGO KWA UJUMLA WAKE,KISIGINO CHA MGUU,VIDOLE VYA MGUU pamoja na MAGOTI.
Tafiti zinaonyesha kwamba, wanawake wanaovaa viatu hivi virefu(high heels) husumbuliwa na Maumivu makali katika maeneo niliyoyataja hapo juu(kiuno,Mgongo,kisigino,vidole vya mguuni n.k), ikiwemo kuathirika kwa Uti wa mgongo pamoja na pingili zake kusagika kwani hufanya kazi kubwa sana ya kujipinda na kuleta balance ya mwili
KUMBUKA; Hakuna mda maalum wa kuanza kuona athari za Uvaaji wa viatu virefu,pengine athari zake huweza kuchukua mda kidogo kutokea, hata siku zikija utashindwa kugundua chanzo ni nini.
Kinga ni Bora kuliko Tiba,Chukua hatua.
Kwa Ushauri Zaidi,Elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!