ZIFAHAMU DALILI 8 ZA KUTOLEWA YAI KUTOKA KWENYE OVARY (OVULATION)

ZIFAHAMU DALILI 8 ZA KUTOLEWA YAI (OVULATION)

Mwanamke anapokuwa kwenye siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ujauzito ambazo hufahamika kama siku za kutolewa kwa yai (Ovulation) huonesha dalili kadhaa zinazotofautiana. Hapa chini kuna dalili 8 zinazotokea kwa wanawake wengi wawapo kwenye kipindi hiki

———————————————————————————

1.Kuongezeka kwa uzalishwaji wa ute usio na rangi (Colourless),mzito,unaovutika na usio na harufu. Kwa baadhi ya wanawake huonekana hadi kwenye nguo za ndani lakini kwa baadhi hubaki ndani na hauonekani kirahisi labda hadi watambue kwa kuingiza vidole


2.Kuongezeka kwa joto la ndani ya mwili hasa kwenye sehemu za siri.Siku hizi wanawake huwa na joto la juu kiasi tofauti na siku zingine za kawaida


3.Mlango wa kizazi hulegea,hutanuka na kuongezeka ubichi kwa kuzalisha majimaji/ute


4.Kuongezeka kwa miwasho kwenye nyonyo/matiti


5.Kuongezeka kwa uwezo wa pua katika utambuzi/kunusa harufu mbalimbali za vitu hasa vyakula,manukato na harufu za wanaume wanaowapenda


6. Hamu ya kushiriki tendo la ndoa huongezeka sana. Nyakati hizi wanawake wengi hujikuta wameshiriki tendo la ndoa na wanaume ambao hawakuwahi kabisa kuwafikiria kabla,na kwa nyakati kadhaa hiki ndicho kipindi ambacho hubadili historia ya wanawake wengi kwa kujikuta wamepata ujauzito usiotarajiwa sababu ya kukosa udhibiti wa haja ya mwili katika kujamiiana na wanaume


7.Maumivu ya nyonga hutokea


8.Tezi mbalimbali za mwili huongeza uzalishaji wa vimiminika vyake mfano mate,jasho n.k


Ukiona dalili hizi zinakusumbua sana jua upo kwenye kipindi hicho,hii inalenga hasa kuwasaidia wale wanawake wasioelewa vizuri mizunguko ya hedhi zao!

Cc; @afyainfo


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!