ZIJUE SABABU ZA TATIZO LA KUHARISHA NA KUTAPIKA

🔻 ZIJUE SABABU ZA TATIZO LA KUHARISHA NA KUTAPIKA

➡️ Kuharisha+Kutapika

Matatizo haya mawili ya kuharisha na kutapika hutokea sana kwa Watu mara kwa mara huku vyanzo vyake vikiwa ni vingi sana.

Sababu za Kuharisha na Kutapika zinaweza kuwa ni Pamoja na Hizi hapa chini;

(1) Sababu za Kichefuchefu na kutapika

- Dalili za magonjwa mbalimbali kama vile Malaria,typhoid,UTI,hormone imbalance(mvurugiko wa vichocheo mwilini) n.k
- Matumizi ya baadhi ya Njia za Uzazi wa mpango,kama vile vidonge,sindano n.k
- Ulaji na allergy ya baadhi ya aina za Vyakula
- Matumizi ya baadhi ya dawa za magonjwa mbalimbali
- Dalili za ujauzito kwa wanawake

N.K

(2) Sababu za kuharisha

- Dalili za Magonjwa mbalimbali kama vile Typhoid,Malaria n.k
- Kula vitu vichafu na kupita moja kwa moja tumboni,Mfano; kinyesi, michanga au uchafu wowote ambao hupita baada ya kula chakula au Maji
- Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huleta hali hii ya kuharisha

KUMBUKA; Sio kila kutapika ni MALARIA, ni vizuri ukihisi hali ya tofauti kwa mwili wako uende kukutana na Wataalam wa afya kwa ajili ya Vipimo na matibabu sahihi Kwako

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!