ZIPI NI DALILI ZA MINYOO? MATIBABU YAKE NI YAPI?
ZIJUE DALILI ZA MINYOO NA MATIBABU YA MINYOO
Minyoo ni nini?
Minyoo huwa inapatikana katika kundi la nematodi(jamii) ambapo makazi yake ni Matumbo ya Binadamu na huweza kusababisha ugonjwa wa minyoo.
Tafiti zinaonyesha kwamba karibu robo ya idadi ya watu duniani wameathiriwa na ugonjwa huu wa minyoo, na ugonjwa huu umeathiri sana katika maeneo ya kitropiki pamoja na maeneo ambayo hali ya Usafi sio Nzuri.
Lakini pia kuna jamii nyingine ya minyoo inayojulikana kama jamii ya Askaris ambayo huweza kusababisha magonjwa katika mifugo.
Jinsi ya Kusambaa na Kuathiri binadamu
Maambukizi ya Minyoo hutokea pale mtu anapokula chakula kilichoathiriwa na kinyesi chenye mayai ya minyoo jamii ya Askaris. Ambapo buu wa mnyoo hutotolewa kisha kujichimbia kupitia utumbo mdogo,
hupenya moja kwa moja mpaka kwenye mapafu kisha kufikia na kuhamia katika mfumo wa hewa. Mnyoo humezwa na mtu na kurudi tena na hukua na kukomaa katika utumbo kwa kuongezeka hadi kufikia sentimita 30 (inchi 12) kwa urefu na hujishikiza katika ukuta wa utumbo.
DALILI ZA UGONJWA WA MINYOO
Maambukizi ya Minyoo huweza kuambatana na dalili mbalimbali kama vile;
- Homa kutokea
- Kuharisha na kuhisi minyoo wakati wa kujisaidia
- Tatizo la Kuvimba tumbo
- Kuvimba ini au wengu
- Tatizo la kichomi cha mara kwa mara
- Kuhisi kichefuchefu na kutapika minyoo ya duara
- Kupata maumivu ya tumbo
- Uzito kupungua
- Endapo minyoo itahamia sehemu nyingine za mwili kama vile mapafu, ini, na sehemu nyingine za mwili huleta madhara makubwa zaidi,mfano kutokea kwa msokoto na kuoza kwa sehemu ya utumbo mdogo ambayo hupelekea kifo.
MATIBABU YA UGONJWA WA MINYOO
Kuna dawa mbalimbali ambazo hutumika kuua minyoo na kutibu tatizo hili ambazo hutolewa hosipitali kwa maelekezo ya daktari kulingana na ukubwa wa tatizo.
* Usisahau kwamba matumizi ya vyoo wakati wa kujisaidia, ulinzi wa chakula dhidi ya uchafu na udongo na kuosha mkono kabla ya kula ni njia mojawapo za kujiepusha na magonjwa ya minyoo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!