Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIPI ZINAWEZA KUWA SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO,MGONGO,NA TUMBO?



KIUNO,MGONGO,TUMBO

• • • • • •

SABABU ZA MAUMIVU YA KIUNO.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kupelekea mwanamke kupata maumivu ya kiuno kwa muda mrefu, sababu hizi ni:


1.Maumbukizi ya ndani ya kiuno ya muda mrefu (Chronic Pelvic Infection)

-kutokana bakteria wa  magonjwa ya zinaa kama kisonono au wadudu wa TB.


2.Endometriosis.

Hii ni hali ambayo seli za ukuta wa uzazi huota sehemu nyingine za uzazi. Huleta maumivu wakati wa hedhi au kufanya mapenzi.


3.Maambukizi ya muda mrefu ya shingo ya uzazi au mji wa uzazi (Chronic endometritis or cervicitis). Husababisha maumivu ya kiuno wakati wowote na wakati wa kufanya ngono.


4.Vivimbe vya kizazi (uterine fibroids)

Husababisha maumivu pale ambapo vinakua kwa haraka, vinajiviringisha au kukandamiza ogani nyingine. Maumivu yake huwa ya kuja na kuacha.


5.Maambukizi ya njia ya mkojo ya muda mrefu(Urinary Tract Infection)

Husababisha maumivu hasa wakati wa kukojoa na chini ya kitovu.


6.Maambikizi ya via vya uzazi(Pelvic inflammatory Disease – PID)


7.Maambukizi ya Kibofu cha Mkojo (Interstitial cystitis) -Hali hii huleta maumivu hasa chini ya kibofu cha mkojo ambayo hupungua pale unapokojoa. Dalili nyingine ni kukojoa mara kwa mara, kukojoa usiku na kushindwa kubana mkojo.


8.Ugonjwa wa Kidole Tumbo(Chronic Appendicitis) -Tatizo la kidole tumbo huleta maumivu upande wa kulia chini ya kitovu ambayo huwa hayatulii na dawa za maumivu.


9.Kushikana KwaVia Vya Uzazi (Pelvic Adhesions)Saratani ya Utumbo Mpana

Tatizo hili huweza kuleta maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu na kiunoni kwa muda mrefu. Via.healthchecktz 


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!






Post a Comment

0 Comments