Ticker

6/recent/ticker-posts

ATHARI ZA KUTOKUNYWA MAJI YA KUTOSHA MWILINI



 MAJI

•••••

ATHARI ZA KUTOKUNYWA MAJI YA KUTOSHA MWILINI


Kuna baadhi ya watu ambao hawajui umuhim wa maji kabsa mwilini, hata kufikia hatua ya kusema wakinywa juic au kinywaji chochote hawaitaji kunywa maji tena.


Chakula kina sehemu yake mwilini, na Maji yana sehemu yake tena kubwa mwilini. 


JE ATHARI ZA KUTOKUNYWA MAJI NI ZIPI?


Kuna athari nyingi za kutokunywa maji au kunywa maji kidogo mwilini,athari hizo ni pamoja na;


• Kupatwa na matatizo ya Figo


• Kupatwa na shida kwenye kibofu cha Mkojo


• Kukusanyika kwa kiwango kikubwa cha sumu mwilini, ikiwemo sumu za Dawa N.K


• Kuleta hali ya makunyanzi katika Ngozi ya mwili pamoja na ngozi kuwa kavu au kuwa ngumu na kukaamaaa


• Kuchangia matatizo ya macho ikiwemo kuuwa nuru katika jicho,hivo kuleta hali ya kutokuona vizuri


• Kuchangia rangi ya macho kubalika na kuwa mekundu


• Kuna uhusiano mkubwa kati ya unywaji wa maji pamoja na kiwango cha damu mwilini,  hivo mtu ambaye hapati maji ya kutosha hupata athari pia katika mzunguko mzima wa damu ikiwa ni pamoja na kiwango cha damu mwilini


• Kupatwa na Matatizo ya kuumwa na kichwa sana


• Hata mzunguko wa hedhi kwa akina Dada huweza kuvurugika kutokana na athari za kutokunywa maji ya kutosha mwilini.


• Kutokunywa maji ya kutosha huweza kusababisha mtu kupata choo kigumu wakati wa kujisaidia au hata kukosa choo kabsa


• Kutokunywa maji huweza kukusababishia mdomo wako kutoa harufu mbaya


• Maji ni muhim sana hata katika afya ya seli hai za mwili


• Mwili kuchoka kupita kiasi


• Kushusha kupita kiwango cha shinikizo la damu mwilini


• Kushambuliwa na magonjwa kama UTI


• N.K


KUMBUKA; Unatakiwa unywe maji angalau kuanzia Lita 2.5 mpaka 3 kwa siku hicho ndyo kiwango cha kawaida.


Tafiti zinaonyesha kwamba,kwa mtu ambaye anakunywa lita 2.5 za maji kwa siku humsaidia kupunguza uwezekano wa kupata UTI za mara kwa mara, kwa zaidi ya asilimia 50%.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






Post a Comment

0 Comments