FANGASI SUGU
•••••••••••
DALILI ZA FANGASI SUGU NA JINSI YA KUZITIBU
Kwanza tuanzie hapa, tukisema fangasi sugu tunamaanisha nini?
Fangasi Sugu; Ni fangasi ambao wamekuwa wakijirudia rudia mara kwa mara na kwa Mda mrefu licha ya kutumia Dawa za aina tofauti tofauti lakini bado wapo.
Mashambulizi ya Fangasi huhusisha maeneo mbali mbali katika mwili wa binadamu Kama vile;
- Kuna fangasi wa Sehemu za siri za mwanamke na mwanaume
- Kuna fangasi wa kwenye Damu
- Kuna fangasi wa kwenye ngozi
- Kuna fangasi wa kichwani
- Kuna fangasi wa kwenye ulimi
- Kuna fangasi wa mdomoni
- Kuna fangasi wa miguuni
- Kuna fangasi wa vidoleni vya mikono na miguu
Wanawake huteswa zaidi na fangasi wa Sehemu za Siri ambapo kwa asilimia kubwa jamii ya Candida Albicans huhusika.
DALILI ZA FANGASI NI PAMOJA;
- Kuwashwa sehemu za siri, kwenye ngozi na hasa katikati ya vidole vya miguuni na mikononi
- Kupatwa na michubuko sehemu za siri pamoja na miguuni
- Kutokwa na uchafu wenye rangi kama maziwa kutoka sehemu za siri za mwanamke
- Kubadilika rangi na kuwa nyekundu kwenye mashavu ya uke,kuzunguka eneo lote la sehemu za siri pamoja na ngozi ya korodani ya mwanaume
- Kutokwa na uchafu kama ukurutu kwenye ngozi
- Sehemu za siri kupata moto sana
MADHARA YA FANGASI SUGU
- Kutokwa na uchafu unaonuka mara kwa mara
- Uke kuwa mkavu na kupelekea maumivu makali wakati wa tendo
- Miwasho inayokera hata ukiwa mbele za watu
MATIBABU
Matibabu ya Fangasi hutegemea eneo,dalili pamoja na chanzo cha Fangasi,hivo ni vzur kuongea kwanza na wataalam wa afya kabla ya kutumia dawa yoyote.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!