DALILI ZA HOMA YA BONDE LA UFA NA MATIBABU YAKE

 HOMA YA BONDE LA UFA

•••••••••


DALILI ZA HOMA YA BONDE LA UFA NA MATIBABU YAKE


Homa ya bonde la Ufa ni ugonjwa ambao unashambulia wanyama pamoja na binadamu lakini kwa asilimia Kubwa huanzia kwa wanyama.

Chanzo cha Ugonjwa huu ni virusi vinavyojulikana kwa kitaalam kama RVF ambavyo huingia kwa wanyama kama mbuzi,kondoo na Ng'ombe na baadae kusambaa kwenda kwa Binadamu.


Ugonjwa huu unaweza usionyeshe dalili zozote mwanzoni na baadae ukaanza kuleta dalili ambazo pia zinaweza kuwa Ngumu kuzitofautisha na dalili za magonjwa mengine.


DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA BONDE LA UFA NI PAMOJA NA;


- Joto la mwili kupanda au kupata Homa

- Mwili kuchoka kupita kiasi

- Kupata maumivu makali kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

- Mgonjwa kukosa hamu ya kula

- Kuonyesha dalili za kuishiwa maji ya mwili, kama ngozi kukamaaa n.k

- Kupatwa na hali ya Mafua

- Mgonjwa kupata kichefuchefu pamoja na kutapika

- Kupata maumivu ya shingo au shingo kukamaaa na kuwa Ngumu.



MATIBABU


Hakuna tiba au dawa maalumu kwa ajili ya kutibu ugonjwa huu wa Homa ya bonge la Ufa, Hivo basi mgonjwa atasaidia matibabu kulingana na dalili anazozionyesha,kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi Mfano; CORONA.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.









0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!