DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA,HISTORIA YAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE

UGONJWA WA EBOLA

•••••••

DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA,HISTORIA YAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE


HISTORIA YA EBOLA

Kwa mara ya kwanza Ugonjwa wa Ebola ulihusishwa kutokea huko ZAIRE(CONGO) mwaka 1976. Ambapo aina tano za Virusi vinavyosababisha Ugonjwa wa Ebola vilikuja kugundulika hapo baadae,baada ya maeneo mengi kuathiriwa na Ugonjwa huu.

NJIA AMBAZO UGONJWA WA EBOLA HUAMBUKIZWA


Ugonjwa huu  huweza kusambazwa kwa njia mbali mbali kama;

- Kupitia kugusana na mgonjwa wa Ebola

- Kupitia maji maji ya mwili wa Mgonjwa,mate,jasho au Damu yake

- Lakini pia Mtu huweza kupata Ugonjwa wa Ebola kwa Kupitia Wanyama pia.


DALILI​ ZA UGONJWA WA EBOLA

Hakuna dalili za Moja kwa moja za Ugonjwa wa Ebola, Japo mgonjwa ataonyesha dalili kama za magonjwa mengine kwani mwili ukipata shida yoyote lazima uonyeshe matokeo, Na dalili hizo ni pamoja na;

  1. Kupatwa na shida ya kukauka kwa koo
  2. Mgonjwa kupata homa pamoja na mwili kuchoka sana
  3. Maumivu makali ya kichwa
  4. Maumivu kwenye joint,misuli pamoja na viungo mbalimbali vya mwili
  5. Ngozi ya mwili kuwasha
  6. Kusikia kichefu chefu pamoja na kutapika
  7. Kupatwa na tatizo la kuharisha
  8. Kupata matatizo ya kwenye Ini
  9. Kupata matatizo ya Figo
  10. Kutokwa na Damu sehemu zote zenye matundu mwilini,kama kwenye masikio,pua na macho.
  11. Hamu ya chakula kupotea
  12. Kupata shida wakati wa upumuaji
  13. Kupata maumivu makali ya kifua
  14. Kubadilika rangi ya macho na kuwa Nyekundu
  15. N.K


VIPIMO VYA EBOLA 

Mgonjwa wa Ebola hufanyiwa vipimo maalum ambavyo huhusisha sampuli za Damu,Mate,jasho N.k kutoka kwa Mgonjwa, Japo mara nyingi vipimo hivo hufanyika baada ya mtu kuhisi ugonjwa huu au kuonyesha baadhi ya Dalili za Ugonjwa huu wa Ebola.


MATIBABU YA UGONJWA WA EBOLA.

Mpaka sasa hakuna matibabu au Dawa ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Ebola. Bali watu hutibu dalili za Ugonjwa kama ilivyo kwa magonjwa mengi yanayosababishwa na Virusi kama CORONA.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!