UGONJWA WA FIGO
• • • • • • •
DALILI ZA UGONJWA WA FIGO
Moja ya viungo muhimu sana katika mwili wa binadamu ni pamoja na Figo, Figo ndyo huhakikisha sumu zote zinazoweza kutolea nje kwa njia ya Mkojo,hupitia hapo. Kwa kawaida binadamu ana Figo mbili upande wa kushoto na kulia, japo kuna watu wachache huzaliwa na Figo moja.
Mtu anaweza kutolewa Figo moja kwa sababu moja au nyingine na akaendelea kuishi,Ingawa haimaanishi kwamba kitendo hicho cha kuwa na Figo moja na kuendelea kuishi kama kawaida kinapoteza thamani ya Figo Mwilini. Moja ya sababu ambazo huweza kusababisha binadamu akatolewa figo ni pamoja na; Figo kushindwa kufanya kazi kutokana na magonjwa mbali mbali,au kutoa figo kwa kupenda kumsaidia mtu mwingine mwenye matatizo ya Figo.
DALILI ZA UGONJWA WA FIGO
Hizi hapa ni baadhi ya dalili ambazo huweza kuashiria kwamba Figo ina Tatizo;
1. Mgonjwa wa Figo huvimba maeneo mbali mbali ya mwili kama vile; Kuvimba miguu,mikono,uso au macho.
2. Mgonjwa kuhisi kizunguzungu na hali ya kutapika kila mara
3. Mgonjwa kukosa usingizi pamoja na mwili kuchoka kupita kawaida
4. Mgonjwa kukamaa misuli ya mwili ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Muscle cramps
5. Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula na kuskia kichefuchefu pamoja na kutapika pia
6. Mgonjwa kuhisi Mkojo kila mara hasa nyakati za Usku
7. Mgonjwa kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu,hii huweza kuwa ishara pia kwamba kwenye figo kuna shida
8. Mgonjwa kupata maumivu kwenye viungo vya mwili,misuli pamoja na joint
9. Tafiti zinaonyesha pia mgonjwa wa figo huweza kupata shida ya kukosa hedhi kama ni mwanamke
10. Ugonjwa wa figo hupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanaume
11. Ugonjwa wa Figo huweza kusababisha mtu kuwa na matatizo ya presha pia, hasa presha ya kupanda
12. Ugonjwa wa figo huweza kusababisha uwepo wa kiwango kikubwa sana cha Potassium kwenye damu, na pia huweza kusababisha matatizo ya moyo kama vile; Moyo kuvimba N.K
MADHARA YA UGONJWA WA FIGO NI PAMOJA NA;
- Kifo
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa kwa mwanaume
- Kupatwa na magonjwa ya moyo
- Kupatwa na matatizo ya shinikizo la Damu au Presha
- Mwili kuvimba ikiwemo uso,macho,mikono na miguu pia
NB; Kama una dalili hizi au unahisi hali ya tofauti ndani ya mwili wako ni vizuri kwenda hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kupata matibabu ya tatizo lako.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!