UKIMWI
• • • • •
DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI
➡️ HIV- Human immunodeficiency virus au kwa kiswahili tunasema Virusi wanaosababisha upungufu wa Kinga mwilini au ukimwi katika mwili wa binadamu
➡️ AIDS- Acquired immunodeficiency Syndrome au kwa kiswahili tunasema, tatizo la upungufu wa kinga mwilini au Ukimwi
Kwa utangulizi tu ni kwamba, Kuna maneno mawili HIV NA AIDS, Ambapo kwa kiswahili maana yake ni Virusi vya Ukimwi(VVU),pamoja na Upungufu wa kinga mwilini ambapo ndyo Ukimwi wenyewe.
CHANZO CHA UGONJWA WA UKIMWI
Hivo basi, Virusi vya ukimwi ambavyo kwa kitaalam huitwa HIV ndivo husababisha tatizo la upungufu wa kinga mwilini/ukimwi ambapo kwa kitaalam tunasema AIDS baada ya kuingia katika mwili wa binadamu.
JINSI VIRUSI VYA UKIMWI VINAVYOSAMBAA
Virusi vya ukimwi huweza kutoka kwa mtu Mmoja aliyeathirika kwenda kwa mwingine kwa Njia zifuatazo;
• Kwa kushare au kushirikiana vitu vyenye Ncha kali kama,Nyembe,sindano N.K, Ndyo maana watu wanaojidunga madawa ya kulevia wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa ukimwi
• Kufanya mapenzi bila kutumia kinga(kondom) au tunasema Ngono zembe kwa tafsri nyingine
• Kufanya mapenzi kinyume na maumbile,watu wanaofanya mapenzi kinyume na maumbile wapo katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa ukimwi
• Kupewa damu ya mtu aliyeathirika wakati wewe huna virusi vya ukimwi
• N.K
WATU WALIOPO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA WA UKIMWI
- Walevi
- Wanaotumia madawa ya kulevia
- Wanaofanyiwa vitendo vya kikatili kama kubakwa au kuingiliwa kinyume na maumbile
- Wanaoshiriki mapenzi kinyume na maumbile
DALILI ZA UGONJWA WA UKIMWI NI PAMOJA NA;
1. Kuanza kupata magonjwa ya mara kwa mara au kuumwa umwa kutokana na kushuka kwa kinga ya mwili,hivo ni rahsi sana mwili kushambuliwa na magonjwa mengine
2. Kupata mafua ya mara kwa mara,Lakini pia sio kila mafua ni ugonjwa huu wa ukimwi
3. Kupata tatizo la kuvimba kwa tezi za maeneo mbali mbali ya mwili kama vile; mapajani,shingoni au kwenye makwapa
4. Kupata homa za mara kwa mara
5. Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi pamoja na mwili kuishiwa nguvu kabsa
6. Kupungua kwa kasi uzito wa mwili
7. Kupata tatizo la kuharisha
8. Kupatwa na hali ya madoa madoa mwilini,kwenye ulimi au mdomoni
9. Kupatwa na hali yakuwa na mapele kwenye ngozi ya mwili
10. Kapatwa na hali ya ukurutu kwenye Ngozi ya mwili
11. Kupatwa na tatizo la kuumwa na kichwa sana
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!