Ticker

6/recent/ticker-posts

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO,MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO, PAMOJA NA VITU VYA KUEPUKA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO



VIDONDA VYA TUMBO

• • • • • •

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO,MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO, PAMOJA NA VITU VYA KUEPUKA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO


1). DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO


Zipo dalili nyingi za vidonda vya tumbo ila dalili kuu ni pamoja na;

- Kupata maumivu makali ya tumbo mara tu baada ya kula hasa vyakula vyenye acid kali kama maharage.


- Kupata maumivu makali ya tumbo baada ya kula pilipili.


- Kupata maumivu makali juu kidogo ya tumbo karibu na chembe moyo, wakati ukiwa na njaa sana au baada ya kula baadhi ya vyakula.


- Kutapika Damu mara baada ya kula chakula huku ikiambatana na maumivu makali ya tumbo


NB; Mtu mwenye Presha pamoja na vidonda vya tumbo hupata shida zaidi.


2). MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO KWA NJIA YA CHAKULA NA DAWA


✓ Nenda hospital kwanza kutana na wataalam wa afya watakushauri dawa salama kwako,na mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana na wagonjwa wa vidonda vya tumbo ni pamoja na OMEPRAZOLE.


✓ Pendelea kula vyakula vyenye asili ya Viazi kwani vina alikaline ambayo husaidia kushusha kiwango cha acid tumboni ambayo ndyo hutonesha vidonda na kukuletea maumivu makali


✓ Pendelea kunywa maji mengi hasa baada ya kuanza kuhisi maumivu ya tumbo


✓ Pendelea kutumia kabegi hasa ile yenye majani ya kijani kilichokolea kwani ndani yake ina ANT-ULCER Vitamin ambazo ni muhumu sana kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo


✓ Pendelea kula matunda jamii ya nyuzi nyuzi hii husaidia sana mfano; machungwa N.k


✓ Jitahidi pia kufanya mazoezi ya mwili


3). MAMBO YAKUEPUKA KAMA UNA VIDONDA VYA TUMBO


• Epuka kula vyakula vyenye acidi sana tumboni mfano maharage


• Epuka matumizi ya Pilipili kwenye chakula au kachumbari


• Usikae na njaa kwa Mda mrefu


• Usipendelee kutumia maziwa kama wengi wanavyodhani kwamba husaidia,kwani CALCIUM iliyopo ndani ya maziwa husababisha ongezeko la uzalishaji wa acid tumboni hivo humuumiza mgonjwa badala ya kumtibu.


• Epuka matumizi ya dawa zenye acid ndani yake Mfano; Mefenamic Acid, ASPRIN n.k


• Msongo wa mawazo au Stress huongeza tatizo,hivo jitahidi kuepuka hali hii kwa kufanya mambo mbali mbali kama; mazoezi kusikiliza mziki N.k


• Epuka matumizi ya Sigara na Pombe


• Epuka matumizi ya vinywaji vyenye Caffeine Nyingi



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.







Post a Comment

0 Comments