FAHAMU KUHUSU MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWA
UCHUNGUZI KWA MTOTO
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWA
Kwa kawaida mtoto anapozaliwa tu anatakiwa kulia, kama asipolia wataalam wa afya wanasema Kuna tatizo, Lakini baada ya mtoto kuzaliwa hata kama amelia,uchunguzi wa kina hufanyika kwa kitaalam tunasema Newborn Examination.
Vitu vingi sana hufanyiwa uchunguzi ili kuangalia kama kuna tatizo lolote kwa mtoto au mtoto yupo sawa ili asijekupata madhara baada ya kuzaliwa,anavyoendelea kukua na hata anapokuwa mtu mzima.
MAMBO MUHIMU AMBAYO MTOTO HUCHUNGUZWA MARA TU BAADA YA KUZALIWA NI PAMOJA NA;
1. Kwanza kabsa kuhakikisha mtoto amelia mara tu baada ya Kuzaliwa,hilo ndyo jambo la kwanza kabsa ambalo hufanyika.
2. Baada ya kitovu cha mtoto kukatwa na kufungwa vizuri,bado uchunguzi wake utaendelea ili kuhakikisha hakuna damu,au kitu chochote cha tofauti kama usaha kinachotoka kwenye kitovu cha mtoto.
Kumbuka; Hairuhusiwi kuweka kitu chochote kwenye kitovu cha mtoto,zile imani za kuweka vitu kama mavi ya ng'ombe kwenye kitovu cha mtoto,ni kuhatarisha tu afya ya mtoto na kumpelekea kupata magonjwa wala hakuna cha zaidi.
3. Macho ya mtoto huchunguzwa,kama kuna dalili zozote za magonjwa kama macho kutoa usaha,N.K. Ingawaje hata kama hakuna dalili za magonjwa kama kaswende au kisonono,bado mtoto atawekewa dawa ya macho ili kumkinga na magonjwa haya.
4. Pua ya mtoto huchunguzwa,kwamba ina matundu mawili kama watu wengine kwa ajili ya kuvuta na kutoa hewa kwa urahisi zaidi.
5. Masikio ya mtoto huchunguzwa na kuangalia kama yanatoa uchafu wowote mfano; Usaha N.K.
6. Sehemu za siri za mtoto huchunguzwa kwa ukaribu zaidi ikiwemo tundu la kutolea Mkojo kama lipo, na kama lipo je lipo sehemu sahihi au lipo sehemu nyingine?,na kama mtoto ni wa kiume,wataalam wa afya huhakikisha korodani zimeshuka kama kawaida.
Kwani endapo mtoto amezaliwa na korodani zipo kwa ndani na hazijashushwa katika hali yake ya kawaida, huweza kuleta madhara makubwa kwa mtoto hapo baadae,Mfano uwezo wa kutengeneza mbegu utaathirika na mtoto kushindwa kumpa mwanamke mimba.
Kumbuka; Korodani kuwa nje au kushuka au kuning'inia,hiii imewekwa kabsa sio bahati mbaya, Lengo ni ili korodani ziwe na joto ambalo litasaidia katika kutengeneza mbegu pamoja na afya ya begu,na joto hili huwa tofauti kidogo na joto la mwili mzima,ndyo maana korodani zinashuka na kuning'inia kwa Nje kidogo.
7. Sehemu ya Haja kubwa ya mtoto huchunguzwa na kuhakikisha sehemu hiyo ipo na mtoto anaweza kujisaidia vizuri.
➡️ KUMBUKA; wapo watoto ambao huzaliwa na sehemu ya haja Kubwa au Sehemu ya haja Ndogo haipo au Imeziba,hivo baada ya tatizo hili kugundulika mtoto hufanyiwa upasuaji mapema na kutibu tatizo hili, Ndyo maana Mama wa mtoto anatakiwa ahakikishe mtoto baada ya kuzaliwa anakojoa vizuri na anajisaidia haja kubwa vizuri.
Kama mtoto anajisaidia kwa shida au hajisaidii kabsa(haja kubwa na haja ndogo) mama wa mtoto hutakiwa kutoa taarifa mapema kwa wataalam wa afya.
8. Joto la mwili la mtoto huendelea kuchunguzwa na kuhakikisha halipandi au mtoto hawi na Homa,Kwani homa ni moja ya dalili za hatari kwa mtoto.
9. Pia kunyonya kwa mtoto huendelea kuchunguzwa,kwani ni lazima mtoto awe ananyonya Vizuri kwa ajili ya afya yake.
Kumbuka; Maziwa ya mama sio lishe tu kwa mtoto bali ni Kinga na Tiba pia Kwa mtoto mdogo, Kinga ya mtoto mdogo dhidi ya magonjwa hutegemea pia maziwa ya mama yake.
10. Baada ya uchunguzi wa kina kwa mtoto,hakikisha pia mtoto wako anaanza kupata Chanjo za magonjwa mbali mbali,Kama vile chanjo ya Kumkinga na ugonjwa wa kifua kikuu au kwa kitaalam hujulikana kama BCG ambazo huanza kutolewa mara tu baada ya mtoto kuzaliwa.
NB; HAKIKISHA UNAHUDHURIA KLINIKI ZOTE ZA MTOTO WAKO,KWA AJILI YA AFYA BORA NA UKUAJI BORA KWAKE.
•
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!