MAGONJWA YA KIFUA
• • • • • •
FAHAMU KUHUSU MAUMIVU YA KIFUA, KIFUA KUBANA, KIFUA KUWA KIZITO
Mtu anaweza kuwa na tatizo la kifua pasipo kujua shida iko wapi, matatizo ya kifua ni mengi kama vile kifua kubana, kushindwa kupumua, maumivu ya kifua, N.k. Matatizo mengine ni ya mda mfupi na mengine ni ya kudumu.
ZIPO SABABU ZA KUWA NA MATATIZO YA KIFUA AMBAZO NI PAMOJA NA;
- Tatizo la kifua linalotokana na Ugonjwa wa homa ya mapafu yaani Pneumonia
- Kuwa na matatizo kama vile kikohozi
- Kuwa na magonjwa ya kurithi vinasaba kutoka katika koo flani kama Asthma
- Kuwa na magonjwa mbali mbali ya moyo ikiwemo na Moyo kuwa mkubwa
- Dalili za magonjwa ya kuambukiza kama Ugonjwa wa CORONA
- Kupata majeraha kwa kuanguka au kupata ajali yoyote inayoumiza kifua
- Kuwa na shida kwenye mirija ya Damu ndani ya mapafu
- Kuwa na tatizo kwenye vifuko vya Hewa ndani ya mapafu maarufu kama Alveoli
- Kuwa na magonjwa mengine kama presha
- Kuwa na ugonjwa wa TB au kifua kikuu
- Shida ya kongosho kuvimba na kutanuka
- Kupata tatizo lolote linalohusu mbavu zako,ikiwemo na shida ya Mbavu kuvunjika
DALILI ZA MTU MWENYE MATATIZO YA KIFUA NI PAMOJA NA;
- Kupata shida sana ya kupumua au kupata tatizo la kukosa hewa na kushindwa kupumua
- Kupata maumivu makali ya kifua
- Kuhisi kuwaka moto ndani ya kifua
- Kupata tatizo la kizunguzungu mara kwa mara
- Kupata maumivu makali ya kichwa
- Misuli ya moyo kukaza
- Kupata hali ya kichefuchefu
- Sauti ya Mgonjwa kukauka au kubadilika kabsa
- Mgonjwa kukohoa mara kwa mara
- Na wakati mwingine kupata shida ya kushindwa kumeza kitu kabsa.
MATIBABU
Moja ya huduma ya kwanza kwa mtu mwenye shida ya kifua hasa yule anayepumua kwa shida, ni kuhakikisha anapata hewa ya kutosha, ikiwemo kuchukua hatua mbali mbali kama vile;
kufungua madrisha yote ya chumba, kumlaza mgonjwa huku kichwa na kifua kimeinuliwa mfano wa mtu anataka kukaaa, pamoja na kuwekewa Oxygen.
Ndipo matibabu mengine yaanze ikiwemo Vipimo mbali mbali pamoja na Dawa baada yakugundua chanzo cha tatizo.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!