IMANI POTOFU ZENYE MADHARA KIAFYA KATIKA MWILI WAKO

 IMANI POTOFU

• • • • •

IMANI POTOFU ZENYE MADHARA KIAFYA KATIKA MWILI WAKO


Watu wengi wameendelea kukumbatia imani potofu ambazo hata zimekuwa chanzo kikubwa cha kuleta athari katika miili yao kwa kujua au kwa kutokujua huku wakiendelea kuzishikilia kwa nguvu zao zote.


Leo tunagusia kuhusu baadhi ya imani hizo potofu pamoja na madhara yake kiafya katika mwili wa binadamu


IMANI POTOFU ZENYE MADHARA KIAFYA KATIKA MWILI WAKO NI PAMOJA NA;


1. Eti ukila mayai wakati wa ujauzito utazaa mtoto ambaye hana nywele, imani hii sio ya kweli na tafiti zinaonyesha ukosefu wa vyakula vya protein kama mayai N.K kipindi cha ujauzito kunaathiri swala zima la ukuaji na maendeleo ya mtoto tumboni pamoja na mama mjamzito. Kumbuka ukosefu wa protein pamoja na madini ya chuma kwa mama mjamzito huweza kumletea madhara kama, shida katika ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na kuwa na tatizo la upungufu wa damu mwilini.


2. Eti ukimkeketa mwanamke hawezi kuwa na tabia za kihuni, hii ni imani potofu na ina madhara makubwa katika mwili wa mhusika, wanawake wengi ambao hufanyiwa kitendo hiki,huanza kuathirikia kisaikolojia pale wanapogundua wao wapo tofauti na wengine, lakini pia madhara ya ukeketaji ni pamoja ma mwanamke kupoteza damu nyingi wakati wa kitendo hiki, kuchanika na kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na hata mwanamke kupoteza maisha kabsa.


3. Eti kula mboga za majani baada ya mama kujifungua huweza kumsababishia tumbo kuwa kubwa zaidi, hii si kweli bali kitendo cha kumnyima mama aliyejifungua mboga za majani unamsababishia ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini ikiwemo VITAMINS, Chakuzingatia tu ni kwamba siku zote mama baada ya kujifungua huanza kula vyakula vilaini na vyenye maji mengi,alafu kadri mda unavyokwenda anaendelea kuchanganya vyakula. Ulaji mzuri wa mama baada ya kujifungua humpa Nguvu,pamoja na kumsaidia kurudisha kiwango cha damu nyingi iliyopotea wakati wa kujifungua hivo kumuepusha mama na tatizo la Upungufu wa Damu mwilini.


4. Eti Kuweka baadhi ya dawa za asili sehemu za siri, humsaidia mama kupata uchungu haraka na kumsaidia asichanike wakati wa kujifungua, kitendo hiki ni hatari sana kwa mama mjamzito na kinaweza kumsababishia madhara makubwa ikiwemo; Mtoto kufia tumboni, mama kuchanika kizazi wakati wa kujifungua kutokana na mgandamizo mkubwa unaosababishwa na dawa hizo bila kujali hali ya mtoto tumboni,mlalo, N.K


5. Eti mtoto akizaliwa na uchafu mama alikuwa anafanya mapenzi sana wakati wa ujauzito, hiyo sio kweli na uchafu huu wakati mtoto anazaliwa kwa kitaalam hujulikana kama Vernix caseosa na unasaidia sana,moja ya faida zake ni kumlinda mtoto tumboni, na kuleta hali ya ulaini ili kuepusha msuguano wakati mtoto akiwa tumboni, lakini pia uchafu huu husaidia kutunza ngozi ya mtoto.


6. Eti kuzaa mtoto alibino ni mkosi katika familia hata kufikia hatua kwa baadhi ya jamii kuwaua watoto hawa japo kwa sasa jamii imeshaanza kuelewa tofauti na zamani,hii ni imani potofu na ualbino ni tatizo ambalo kitaalam husababishwa na ukosefu wa kichocheo cha Melanin,ambacho kazi yake kubwa ni kuipa Ngozi Rangi yake.


MADHARA YA IMANI HIZI POTOFU NI PAMOJA NA;


- Kusababisha Ugomvi katika jamii


- Kusababisha hali ya msongo wa mawazo


- Kusababisha madhara katika afya ya mwili kama mwili kudhoofika,kukosa nguvu n.k


- Kusababisha vifo katika jamii


- Kuleta hali ya unyanyapaa ndani ya jamii



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!