JE KUNA FAIDA YOYOTE YA KUPIGA CHAFYA KWENYE MWILI WA BINADAMU?

 KUPIGA CHAFYA

• • • • • 

JE KUNA FAIDA YOYOTE YA KUPIGA CHAFYA KWENYE MWILI WA BINADAMU?


Wakati mwingine unatakiwa ufahamu kwamba Chafya ni afya, hivo usizuie kupiga chafya kwani mwili wako upo kwenye hatua ya kuleta afya.


Fahamu kwamba mwili wa binadamu upo katika hali ya ulinzi  thidi ya kitu chochote kipya kinachoingia ndani kwa mda wowote, hata kama wewe ukiwa katika usingizi mzito. Na moja ya vitu vinavyoonyesha kwamba mwili unafanya kazi kupambana na kitu chochote kigeni kinachoingia ndani ni kupiga chafya.


FAIDA YA KUPIGA CHAFYA


-Upigaji wa chafya husaidia kuondoa kitu chochote kigeni kinachojaribu kuingia mwilini kwa Njia ya hewa,Mfano; vumbi N.K.

- Hivo upigaji chafya husaidia vitu hivi visiweze kuingia ndani katika mfumo wa hewa,bali mtu aendelee kuvuta hewa safi tu na si kitu kingine.


Wengine wakiingiwa na vitu kama vumbi katika mfumo wa hewa huanza kuhisi hali ya tofauti,pua kuwasha,hali ya kama kuwa na mafua,koo kuwasha, N.K ,lakini baada ya kupiga chafya tu hujihisi hali ya kawaida na salamaa zaidi.


Hyo tafsiri yake ni kwamba mwili umegundua kuna kitu kigeni(vumbi) kimeingia ndani, na baada ya kupiga chafya kimetolewa Nje.


Lakini pia hali ya kupia chafya huweza kuletwa na vitu vingine mbali na vumbi, kama maambukizi ya Virusi au Bacteria katika Mfumo wa hewa.


Asante kwa kunielewa, lakini pia kama una maoni au swali niandikie hapo chini kwenye Uwanja wa Comment ili twende Sawa. au.!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUNAWEZA KUWASILIANA KWA NAMBA +255758286584.










0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!