Ticker

6/recent/ticker-posts

JINSI YA KUPUNGUZA HALI YA KIUNGULIA(HEARTBURN) KWA MAMA MJAMZITO



KIUNGULIA(HEARTBURN)

• • • • • •

JINSI YA KUPUNGUZA HALI YA KIUNGULIA(HEARTBURN) KWA MAMA MJAMZITO



Kutokana na mabadiliko mengi mwilini yanayosababishwa na mabadiliko ya vichocheo vya mwili wakati wa Ujauzito,Mama Mjamzito amekuwa akikumbwa na matatizo au shida mbali mbali kama vile; Kutema mate mara kwa mara,kupata choo kigumu, kutokupenda baadhi ya vyakula,kichefu chefu na kutapika,kukosa usingizi,Kukojoa mara kwa mara pamoja na Kusumbulia na KIUNGULIA Kikali wakati wa Ujauzito.


Leo tutazungumzia kuhusu shida hii moja ya kiungulia wakati wa Ujauzito pamoja na Njia za kumsaidia mama mjamzito mwenye shida hii.


JINSI YA KUPUNGUZA HALI YA KIUNGULIA(HEARTBURN) KWA MAMA MJAMZITO


• Usikimbilie kwenda kulala mara tu baada ya kumaliza kula, tenga mda wa kusubiri kidogo  angalau dakika 45 ndipo ujiandae kwenda kulala.


• Hakikisha wakati wa kulala kichwa hakiwi chini sana,kwani hali hii huweza kusababisha acid iliyopo tumboni kupanda na kurudi juu hivo kusababisha hali ya kiungulia kwa urahisi sana, hivo unashauriwa kutumia vitu kama mto ili kuinua kichwa kidogo wakati wa kulala.



• Matumizi ya vitu kama  matunda yenye asili ya nyuzi nyuzi kama maembe, na machungwa, Maziwa,maji ya vuguvugu na asali pia huweza kusaidia tatizo hili.


• Kula chakula kidgo kidgo ila mara kwa mara ili kuepuka tumbo kujaa sana,kwani hali hii ni rahisi kusababisha gesi pamoja na acid kurudi kwa haraka kwenda juu,na kupelekea mama Mjamzito kupata kiungulia kikali mara kwa mara


• Matumizi ya maji ya kunywa ni muhim sana ila usinywe mengi kwa wakati mmoja hasa hasa wakati unakula.


• Epuka kabsa matumizi ya pombe au Sigara ukiwa Mjamzito


• Pia usipendelee  kula sana vyakula vinavyoleta gesi sana tumboni na vyenye acid nyingi kama Maharage,kula kiasi.


NB; Epuka matumizi ya dawa hovio ukiwa mjamzito pasipo maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya. 


Kwani sio kila dawa ni salama kwako pamoja na ujauzito uliobeba tumboni.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.








Post a Comment

0 Comments