KANSA YA KIBOFU CHA MKOJO
.........
KANSA YA KIBOFU CHA MKOJO,DALILI ZAKE PAMOJA NA MATIBABU YAKE
Katika mwili wa Binadamu kuna aina nyingi za Kansa Ikiwemo hii ya kibofu cha Mkojo ambayo tunaizungumzia hivi Leo. Kansa hizo ni pamoja na;
- Kansa ya Damu
- Kansa ya Ngozi
- Kansa ya Mapafu
- Kansa ya Koo
- Kansa ya utumbo
- Kansa ya shingo ya Kizazi
- Kansa ya matiti
- Kansa ya kizazi
- Kansa ya Ini
- Kansa ya Ubongo
- Kansa ya Tumbo
- Kansa ya kibofu cha Mkojo
- Kansa ya Mifupa
- N.K
Hivi leo tutazungumzia kuhusu aina hii ya kansa ya kibofu cha Mkojo,Je dalili zake ni zipi? na matibabu yake ni yapi?
Kama lilivyo neno lenyewe,Kansa hii hutokea kwenye kibofu cha mkojo, na endapo itatokea Mgonjwa atapata Dalili zifuatazo;
- Mgonjwa kupatwa na shida ya maumivu makali sana wakati wa kukojoa
- Mgonjwa kupatwa na shida ya kukojoa Damu wakati wa kujisaidia haja ndogo
- Kupatwa na uvimbe ambao hujitokeza kwa ndani ya kibofu cha mkojo au Urinary bladder kwa kitaalam
- Kupatwa na tatizo la kushindwa kuuzuia Mkojo kutoka
- Kupatwa na tatizo la maumivu makali ya Mgongo
- Kuhisi haja ya kujisaidia haja ndogo au mkojo kila mara lakini Mkojo hutoka mdogo sana
- Aina hii ya kansa pia huweza kuleta tatizo la mgonjwa kuishiwa na Damu mara kwa mara
- Maumivu ya tumbo hujitokeza pia kwa Mgonjwa mwenye Saratani hii ya kibofu cha Mkojo
MATIBABU
Kama zilivyo kansa zingine,urahisi wa matibabu ni pale ambapo ugonjwa huu umegundulika mapema kabla ya kufikia stage mbaya,Kwani ikifikia stage mbaya hata kutibu pia ni vigumu. Hivo pale ukijihisi tofauti pamoja na kuona dalili nilizozitaja hapo juu wahi hospital kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584
afya
afyaclass
afyatips
magonjwa
magonjwa ya wanaume
magonjwa ya wanawake
magonjwa ya watoto
makala
mpya
muhimu
new
post
uzazi
0 Comments
WEKA COMMENT HAPA..!!!