MADHARA YA BAADHI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO

• • • • • •

MADHARA YA BAADHI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO


Zipo njia Nyingi za Uzazi wa Mpango,na Njia hizo zimegawanyika katika makundi mbali mbali kama Ifuatavyo;



(A). KULINGANA NA ASILI


Kulingana na asili tuna njia za uzazi wa mpango katika makundi haya mawili;


1. NJIA ZA ASILI(TRADITIONAL METHODS)


- Hapa tunazungumzia matumizi ya njia kama KALENDA katika kupanga Uzazi


2. NJIA ZA KISASA(MODERN METHODS)


- Hapa tunazungumzia matumizi ya njia kama Njiti,Kitanzi au Vidonge katika kupanga uzazi


(B). KULINGANA NA MUDA


Kulingana na Muda tuna makundi matatu ya Njia za Uzazi wa Mpango kama ifuatavyo;


1. NJIA ZA MUDA MFUPI


Hapana tunazungumzia matumizi ya njia kama KONDOM(kike&kiume), Na VIDONGE vya Majira katika kupanga uzazi


2. NJIA ZA MUDA MREFU


Hapana tunazungumzia matumizi ya njia kama, SINDANO, NJITI, AU KITANZI katika kupanga uzazi


3. NJIA ZA KUDUMU


Hapana tunazungumzia KUFUNGA UZAZI kabsa kwa MWANAUME NA MWANAMKE katika kupanga uzazi



MADHARA YA BAADHI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO


1. MADHARA YA VIDONGE VYA MAJIRA


- Kuumwa na kichwa cha mara kwa mara


- Kubadilika kabsa kwa Mzunguko wa hedhi kutokana na vichocheo vilivyopo ndani ya vidonge hivi


- Kupata blid ambayo inatoka nyingi na kwa mda mrefu kidgo


- Kupatwa na hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara


- Wengine hupoteza hamu ya kula kabsa


- N.K



2. MADHARA YA SINDANO


- Mwanamke kukaa mda mrefu bila kushika mimba au Ujauzito pale atakapohitaji kubeba mimba


- Kuumwa na kichwa cha mara kwa mara,pamoja na kichefuchefu


- Mwanamke kublid damu nyingi na kwa Mda Mrefu Mfano; Zaidi ya wiki moja mfululizo


- Mwanamke kukosa period kwa Mda mrefu Mfano; zaidi ya miezi miwili na kuendelea


- Sindano hulainisha mifupa ya mwili,hivo kumuweka mwanamke katika hatari ya kuvunjika mifupa kwa urahisi zaidi


- kubadilika kabsa katika mzunguko wa hedhi,ikiwa ni pamoja na mzunguko kukosa tarehe maalum na damu kutoka vitone vitone.


3. MADHARA YA NJITI


- Kubadilika katika Mzunguko wa hedhi ikiwa ni pamoja na kukosa tarehe maalum za hedhi kutoka.


- Maumivu makali ya kichwa cha mara kwa mara


- Kupata blid ya vitone vitone pasipo mpangilio maalum


KUMBUKA; Matumizi ya Njia za uzazi wa mpango hutofautiana kati ya mtu na mtu kulingana na mwili wake pamoja na uzazi anaopanga, Hivo basi ni Vizuri kukutana na wataalam wa afya ili kukushauri Njia Salama kwako kulingana na mwili wako,Sio kwa sababu rafki yako anatumia aina hyo ya uzazi wa Mpango.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comments

WEKA COMMENT HAPA..!!!